- Corazon alimshukuru mpenzi wake au baba wa watoto wake kwa kuwa rafiki yake wa karibu na mfumo mkubwa wa usaidizi.
Frankie ambaye ni mwaimu wa mazoezi, anaadhimisha miaka 32 hii leo, na kupitia kwenye ukurasa wa mpenzi wake wa instagram Corazon amemtakia heri njema ya kuzaliwa.
Corazon alimshukuru mpenzi wake au baba wa watoto wake kwa kuwa rafiki yake wa karibu na mfumo mkubwa wa usaidizi.
Mtoto wao wa kike amefikisha mwezi mmoja tu na mzaliwa wao wa kwanza ana mwaka mmoja. Corazon anakiri kwamba mara ya kwanza alipomuona Frankie, alijua wangekuwa marafiki wakubwa lakini waligeuka kuwa wapenzi.
"Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu @frankie_justgymit . Wewe ndiye mtu mtamu zaidi, mkarimu, mvumilivu ninayemjua
Asante kwa kuwa rafiki yangu bora na mfumo mkubwa wa usaidizi. Nilipokutana nawe nilijua mara moja tutakuwa marafiki milele
Nina furaha wakati umetufikisha hapa; sasa wazazi wa mvulana mtamu zaidi na msichana mpole zaidi
Unapofikisha miaka 32 na utimize yote ambayo moyo wako unatamani. Uendelee kukua katika upendo, imani na wema. Mungu awapiganie vita vyenu na awatetee hata katika vita vyenu vikali," Aliandika Corazon.