Siogopi kusema hadharani nakupenda-Nyota Ndogo kwa mumewe

Muhtasari
  • Licha ya wawili hao kukosana mwaka jana, na kusuluhisha mambo yao, mapenzi yao yanaonekana kunoga kila kuchao
Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Msanii maarufu kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemlimbikizia mumewe sifa tele, kwa ajili ya mapenzi yake.

Nyota amekuwa akivuma mitandaoni, kwa jambo moja au nyingine.

Haya yanajiri siku chache baada ya msanii huyo kuwaonya wanamitandao dhidi ya kumweka kwenye jumbe za wazungu kuwauwa wapenzi wao waafrika.

Licha ya wawili hao kukosana mwaka jana, na kusuluhisha mambo yao, mapenzi yao yanaonekana kunoga kila kuchao.

Nyota na mumewe wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 5 na kwa kawaida hajaikuwa safari rafisi, huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa alimnakilia ujumbe wa kipekee.

"Mimi nakupenda sana na unajua my love.siogopi kusema hadharani nakupenda.your stone face loves you so much.hio jina ulilonipa na ndio unaniitaga MY STONE FACE.jamani mume wangu anasemaga uwa sichekagi nakuaga stone face.ama ndio hio sura yangu.HAPPY BIRTHDAY MY HUSBAND.I love you."