'Ni pigo zito,'Lulu Diva awashukuru waliosimama naye baada ya kumpoteza mama yake

Muhtasari
  • Lulu Diva awashukuru waliosimama naye baada ya kumpoteza mama yake
Lulu Diva
Lulu Diva
Image: INSTAGRAM

Kumpoteza mtu umpendaye au jamaa yako ni jambo ambalo sio rahisi katika maisha ya mwanadamu.

Msanii kutoka Tanzania Lulu Diva kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashukuru, mashabiki,marafiki,wasanii kwa kusimama naye wakati alipokuwa akikumbana na kipindi kigumu maishani mwake.

Leo ni siku ya Pili Sasa Tangu KUMALIZA arobaini ya msiba wa Mama yangu nikaona haitakuwa busara kama sitachukua nafasi hii kutoa neno la shukurani, kutoka moyoni mwangu napenda kutoa SHUKRANI ZANGU ZA DHATI kwa wote waliokuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu, upendo mlionionesha ni mkubwa mnoo, nikiri SIKUUTEGEMEA, na niseme tu Namshukuru MUNGU sana kwa ajili yenu, mmenifariji sana!!!!

Hii ni kwa kila mmoja aliejitoa juu yangu kwa hali na mali, Wasanii wenzangu, Viongozi mbalimbali, Vyombo vya habari, Wadau tofauti, Mashabiki zangu, ndugu, jamaa marafiki na Watanzania wote walioguswa kwa ujumla, iwe kwa kuja kuniona, kwa kunipigia simu, kwa kusafiri na mimi, kwa post za faraja na kwa namna yoyote ile, kutoka moyoni mwangu kabisa nawashukuru sana sana WOTE na NINATHAMINI 🙏."

Kulingana na msanii huyo kumpoteza mama yake imekuwa pigo kubwa katika maisha yake.

"Nikiwa kama mtoto pekee kwa Mama yangu Ukaribu wetu haukuwa wa kawaida, nakiri NIMEONDOKEWA!! kwangu hili ni PIGO zito,

Na kiubinaadamu maumivu yake hayaelezeki, lakini pamoja na yote MUNGU ametuagiza tushukuru kwa nyakati zote hivyo namshukuru kwa kila jambo na sina complain yoyote juu ya kazi yake, yeye ndio alietoa na yeye ndio alietwaa!!

Kuendelea kukaa ndani sio kitu ambacho hata Mamaangu angependa, maisha lazima yaendelee ukizingatia nina kazi na watu wengi ambao wamenipa muda wa kutosha na kuna mengi binafsi yako mbele yangu kwasasa, Mama hayupo lakini MUNGU yupo!! Yeye aliemchukua ndio atajua namna gani atanifariji," Alisema Lulu.