Kizuri cha jiuza,'Massawe Japanni amtetea Jalang'o dhidi ya madai ya VDJ Jones

Muhtasari
  • Kizuri cha jiuza,'Massawe Japanni amtetea Jalang'o dhidi ya madai ya VDJ Jones

Mtangazaji wa Radiojambo Massawe Japanni, amejitokeza wazi wazi na kutetea Jalang'o dhidhi ya madai yake VDJ Jones kwamba ameua muziki wa Gengetone.

VDJ Jones alimsuta vikali mtangazaji Willy M Tuva na Jalang'o kwa kile alichokitaja kuzima ndoto za wasanii wengi wa muziki wa Gengetone.

Massawe amesema kwamba Jalang'o sio wakulaumiwa kwani baadhi ya wasanii wa gengetone hawatoi muziki ambao unaweza kuchezwa hewani na watangazaji.

"UPUUZI!! Mbona wasanii wote wa gengetone hawalii???? Kizuri chajiuza,Fanya bidii studioni na acha kutarajia uchezaji wa hewani kwa utayarishaji duni @jalangoo kuapishwa saa 10.05 asubuhi usiogope kaka!"lisema Massawe.

Ifahamike kwamba VDJ Jones alitangaza kwamba atakuwa anawania kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi huku akisema kwamba kushinda uchaguzi mgombea anahitaji kuwasilisha manifesto yako na wala sio kuwa na hela nyingi.