'Maisha hayaji na mwongozo,'Akothee amshauri mwanawe Vesha

Muhtasari
  • Mama huyo wa watoto watano amefurahishwa sana na ubora wa bintiye kwani huwa anang'ara katika masomo
  • Pia ameandika kipande cha ushauri akimtaka Vesha kuwa na mipango yake binafsi na asitegemee mtu yeyote kumfanyi
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Esther Akoth almaarufu Akothee ni gwiji maarufu wa mitandao ya kijamii na msanii mkubwa wa muziki anayejulikana kote nchini.

Mama huyo mashuhuri alianza kazi yake ya muziki muda mrefu na amefanya vyema katika fani hiyo, na kuifanya tasnia ya burudani kuwa nyepesi.

Akothee hufanya uundaji wa maudhui ikijumuisha matangazo, mazoezi na mafunzo ya upishi.

Akothee ni mama wa watoto watano, mpenzi wake wa sasa ni Nelly Oaks. Wapenzi hao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na ni dhahiri uhusiano wao huwa wa kufurahisha kila wakati.

Kwa hivyo leo Akoth ameweka picha yake akiwa na bintiye Vesha. Binti zake wote wamehitimu katika vyuo vikuu na sasa anangojea digrii ya pili kutoka kwa Vesha.

Mama huyo wa watoto watano amefurahishwa sana na ubora wa bintiye kwani huwa anang'ara katika masomo.

Pia ameandika ushauri akimtaka Vesha kuwa na mipango yake binafsi na asitegemee mtu yeyote kumfanyia.

"Maisha hayaji na mwongozo, yanahusiana na mwingine @veshashaillan weka kichwa chako juu zaidi ya matarajio ya ulimwengu. Hakuna aliye na mipango kwako bora uwe na mipango yako mwenyewe, Watu wanaona thamani ndani yako na hicho ndicho kinachovutia kwenye mafanikio. Siwezi kusubiri shahada hii ya pili nyarkamagambo @veshaillan."