'Sitafuti kiki,'Nandy akiri baada ya kupakia ujumbe wa kuachwa

Muhtasari
  • Aidha alisema kwamba yeye sio msanii wa kiki, na kwamba anazungumzia hayo kwa ajili ya watu wengi wanaopitia maumivu ya mapenzi

Msanii kutoka Tanzania Nandy amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kuandika ujumbe akizungumzia mapenzi na jinsi yanaumiza.

Nandy alisema kwamba ataongea kile kinamuumiza na wala asihukumiwe na mtu yeyote.

Aidha alisema kwamba yeye sio msanii wa kiki, na kwamba anazungumzia hayo kwa ajili ya watu wengi wanaopitia maumivu ya mapenzi.

"Mara kiki...mara pole mara hivi mara vile jamani nitaongea nitasema kinacho niumiza msinihukumu kabla sijaongea 

Mimi sio msanii wa kiki najiamini muziki wangu, ila haya yote nina yofanya ni kwa ajili ya watanzania wote wanaopitia maumivu makali ya mapenzi," Nandy amesema.

Haya yanajiri baada ya msanii huyo kukejeliwa na wanamitandao ,baada ya kupakia ujumbe akidai kwama amechoka na mapenzi.

wezi jana Nandy alivishwa pete ya uchumba na mpenziwe Billnass.