Kanye West afungiwa Twitter kwa muda kwa kuchochea ghasia

Bosi mpya wa Twitter Elon Musk aliombwa na mtumiaji mmoja "kumchukulia hatua Kanye".

Muhtasari
  • West alikuwa "amekiuka sheria yetu dhidi ya uchochezi wa ghasia", Musk alitweet
Image: Instagram Kanye West

Kanye West amefungiwa kwenye Twitter kwa shutuma za "kuchochea vurugu" kufuatia machapisho ya kuudhi aliyoweka mtandaoni - miezi miwili tu baada yakuondolewa kwa marufuku yake ya mwisho.

Rapa huyo wa Marekani, ambaye sasa anafahamika kwa jina Ye, alichapisha mfululizo wa tweets zisizokuwa na uhakika - moja kati ya hizo zilionekana kuwa na ishara inayochanganya swastika na nyota wa Kiyahudi.

Bosi mpya wa Twitter Elon Musk aliombwa na mtumiaji mmoja "kumchukulia hatua Kanye".

West alikuwa "amekiuka sheria yetu dhidi ya uchochezi wa ghasia", Musk alitweet.

"Akaunti itafungiwa kwa muda," Musk aliandika katika chapisho la Twitter.