Aliyekuwa muigizaji wa Selina, Lenana Kariba na mkewe mzungu wabarikiwa mtoto wa kwanza

Muigizaji huyo alishiriki picha ya binti yake Ava huku akimshika mkono na kuandika.

Muhtasari

•Huku akitangaza habari hizo njema kwenye mitandao yake ya kijamii; muigizaji huyo alishiriki picha ya binti yake Ava huku akimshika mkono na kuandika.

•Muigizaji huyo wa zamani wa Selina alifichua kuwa anataka watoto wake wasome nchini Uingereza.

Lenana Kariba na mkewe mrembo.
Lenana Kariba na mkewe mrembo.
Image: HISANI

Muigizaji wa Kenya Lenana Kariba na mkewe ni wazazi wapya zaidi mjini baada ya kumpokea mtoto wao wa kwanza.

Huku akitangaza habari hizo njema kwenye mitandao yake ya kijamii; muigizaji huyo alishiriki picha ya binti yake Ava huku akimshika mkono na kuandika.

"Hamjambo wallimwengu..Kutana na Ava   "

Muigizaji huyo wa zamani wa Selina katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye Instagram alifichua kuwa anataka watoto wake wasome nchini Uingereza.

Lenana alifichua kwamba mkewe amekuwa akitamani tufaha na maembe.

Kulingana na Lenana, wanataka kujaribu na kuhakikisha wanapata uzoefu wa maisha katika nchi zote mbili, Kenya na Uingereza.

"....Tutaendelea kusafiri kwenda na kurudi. Shule tunapanga kwenda Uingereza lakini basi, kila likizo tutatoka kwa ndege. Nahitaji wazazi wangu wawafundishe Kikuyu," alisema.

Aliongeza kuwa yuko tayari kufanya bidii katika uzazi na kuwa mwangalifu sana kumpa mtoto wake bora awezavyo.