Mume wa mzazi mwenzake Harmonize amsherehekea binti yake Zuuh Konde kwa ujumbe maalum

Bintiye Harmonize, Zuuh Konde anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya tano.

Muhtasari

•Malkia huyo mdogo anasherehekea miaka mitano tangu alipoletwa humu duniani na mama yake Official Shanteel.

•Baba wa kambo wa Zuuh, Captain Tango pia hakuachwa nyuma katika kumsherehekea kwa ujumbe mzuri wa heri ya siku ya kuzaliwa.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Leo, Mei 30, mtoto wa pekee wa staa wa Bongo Harmonize, Zulekha Rajabu almaarufu Zuuh Konde anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Malkia huyo mdogo anasherehekea miaka mitano tangu alipoletwa humu duniani na mama yake Official Shanteel.

"Nakupenda. Mungu wangu akulinde Konde Queen. Heri ya siku ya kuzaliwa boss lady," Harmonize alimsherehekea bintiye kwenye Instagram.

Shanteel ambaye ni mfanyibiashara wa samani pia alimsherehekea bintiye na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Happy birthday mwanangu kipenzi nakupenda sana @zuuh_konde," alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baba wa kambo wa Zuuh, Captain Tango pia hakuachwa nyuma katika kumsherehekea kwa ujumbe mzuri wa heri ya siku ya kuzaliwa.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Tango alichapisha video yake na Zuuh wakiburudika na kucheza pamoja ndani ya nyumba.

"Happy birthday @zuuh_konde. Uncle Tango anakupenda sana. Chap nakuja na zawadi @official_shanteel hongera," alisema.

amemsherehea binti yake wa Kambo Zuuh Konde
Capt Tango amemsherehea binti yake wa Kambo Zuuh Konde
Image: INSTAGRAM// CAPT TANGO

Mjasiriamali huyo alimtambua binti huyo wa Harmonize kama mwenye busara sana. Bi Official Shanteel alifunga pingu za maisha na mume wake Captain Tango mwezi uliopita baada ya kuchumbia kisiri kwa muda.

Mapema mwaka huu, Harmonize alidokeza kuhusu hatua ya binti yake wa pekee kujiunga na shule ya chekechea.

Konde Boy alionyesha video ya yeye, baby mama wake, bintiye na mwalimu baada ya kulipa karo ya shule na kuandika:

"Nifanye nijivunie. Niko hapa kwa ajili yako. Baba anakupenda, sawa ni wakati wa shule," aliandika chini ya video hiyo.

Official Shanteel alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmonize wakati mwanamuziki huyo alikuwa bado akichumbiana na Sarah Michelloti. Uhusiano huo wa kipindi kifupi ulifanya wawili hao kujaliwa mtoto mmoja  wa kike pamoja, Zulekha Nasra (Zuuh Konde) na pia ulivunja ndoa ya bosi huyo wa Kondegang na Sarah.

Mwaka wa 2021, Harmonize alipokuwa akizindua albamu yake  'High School' alifunguka kuhusu utata uliozingira kuzaliwa kwa bintiye.

Mwimbaji huyo alifichua kwamba kuzaliwa kwa mtoto huyo ndicho chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake ya kwanza na Sarah Michelloti.

Harmonize alisema ndoa yao ya miaka minne ilianza kusambaratika wakati mpenzi wake alikuwa amesafiri kuenda kwao na baada ya kuwa pweke kwa muda akapata majaribu ya kutembea na mwanadada aliyemzalia mtoto.

"Ilikuja kipindi akawa anasafiri kuenda kwao. Nilikuwa Tanzania na kama unavyojua umbali wa mapenzi unapokuwa nikaishia kutembea na mwanamke ni mama Zuuh sasa hivi. Kwa mipango ya mwenyezi Mungu nikamfanya mjamzito." Harmonize alisema.

Konde Boy alifichua kwamba Shanteel alikuwa na wasiwasi kuhusu ujauzito huo na hata alikuwa tayari kuutoa ila akamkataza.

Alisema kuwa alikubali majukumu na akahudumia ujauzito ujauzito hadi mtoto alipozaliwa