Akothee akumbuka jinsi Sonko alivyomsidia huku akimpongeza kwa kumsaidia Conjestina

Msanii huyo alieleza jinsi Sonko alimsaidia baada ya kukutana naye.

Muhtasari
  • Akothee ​​alikutana na Sonko mwaka wa 2019 alipokuwa Turkana akisambaza chakula na wakapatana hotelini.
Esther Akoth

Mjasirimali na msanii Esther Akoth almaarufu Akothee kupitia ukurasa wake wa instagram amfichua jinsi alivyopatana na Mike Sonkomara ya kwanza  baada ya kubadilisha maisha ya Congestina na kumpa kazi.

Msanii huyo alieleza jinsi Sonko alimsaidia baada ya kukutana naye.

Akothee ​​alikutana na Sonko mwaka wa 2019 alipokuwa Turkana akisambaza chakula na wakapatana hotelini.

Baada ya Sonko kuona msafara mkubwa sana na kuuliza ni nani mwingine alikuwa karibu naye alifahamishwa kuwa Akothee alikuwa hapo.

Sonko alimpigia simu  ​​na kumpa laki moja ya mafuta ya magari yake ambayo yalichangia pakubwa katika kazi zake za hisani.

"Niruhusu Nimthamini Janeko wangu. Watu wazimu wana mambo sawa. Mioyo mikubwa. Mnamo mwaka wa 2019 nikiwa Turkana nikisambaza chakula, tukakutana katika hoteli moja na Mhesh Mike Sonko Kisha akanipigia simu na kunipa ksh 100,000 Maneno yake "Sema mrembo ,naona uko na team kubwa and your logistics must be crazy , chukuwa hii 100,000 ksh weka nayo mafuta , unataka Unga ama maziwa nikuongezeee ? Akaniongezea na Lori MOJA ya Unga Tukalisha Turkana ."

 Kwa hivyo aliweka wazi kwamba Mike Sonko hawasaidii watu kwa ajili ya PR au kupata usikivu bali yeye hufanya hivyo kutoka moyoni mwake.

Alimalizia kwa kumshukuru Sonko kwa kumrudisha Congestina maishani ambayo ni Mungu pekee anayeweza kumlipa.

" @mike.sonko hafanyi PR na Charity, ni mfadhili wa kweli, hana kichaa, ni Mwaminifu, watu waaminifu wanaonekana kama watu wazimu wanasema mambo waoga na wanafiki hawasemi.

Leo ninapomtazama akibeba congestina maishani 🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏😭😭😭." ITS ONKY GOD Wakati baadhi yetu wanachepuka, Niruhusu NIMPONGEZE MPENZI WANGU MIKE SONKO. MUNGU AKUBARIKI SANA . Sonko hana hata timu ya wanahabari inayomfuata kama viongozi wengine serikalini wanaozunguka kwa madhumuni ya PR. His things are authentic.he is doing him , sonko kama Kuna Mbingunj Cha ukweli , sitashtuka kukutana na wewe huko 🙏 Ubarikiwe sanaaaaaa @mike_sonko,"Akothee alimpongeza.