"Ni mkarimu ila mkali!" Nyamu afichua maelezo ya mrembo aliyemfariji Sakaja kwa upendo

Wakenya wamekuwa na hamu ya kutaka kumjua ZAIDI MCA huyo ambaye alionekana akimtuliza gavana Sakaja siku ya Jumanne.

Muhtasari

•Seneta Karen Nyamu pia anajulikana kama Suzzy au Makush na alizaliwa katika mtaa wa mabanda wa Mathare.

•Seneta huyo wa UDA alifichua kuwa ana uhusiano wa karibu na Bi Makungu na kumtaja kama "msichana wangu."

akifarijiwa na MCA wa Mlango Kubwa Susan Makungy huku akimwaga machozi Roysambu, Nairobi mnamo Juni 20, 2023.
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja akifarijiwa na MCA wa Mlango Kubwa Susan Makungy huku akimwaga machozi Roysambu, Nairobi mnamo Juni 20, 2023.
Image: SCREEN GRAB

Siku ya Jumatano, seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu alitoa maelezo kuhusu mrembo ambaye amekuwa gumzo mitandaoni baada ya picha zake akimfariji gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Facebook, Karen Nyamu alibainisha kuwa Wakenya wengi wamekuwa na hamu ya kutaka kujua mwanamke huyo ni nani na ana uhusiano gani na gavana Sakaja.

“Huyu ni MCA wa Wadi ya Mlango Kubwa ambaye aliharakisha kutuliza hisia za Gavana Sakaja jana (Jumanne) alipolemewa na hisia wakati alipokuwa akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa kaunti ya Dishi na. Kwa sasa anatrend kwenye mitandao ya kijamii, na kwa sababu watu wengi wameniuliza yeye ni nani..,” Nyamu alimtambulisha mrembo huyo.

Nyamu aliendelea kufichua kwamba MCA huyo aliyechaguliwa kwa tikiti ya UDA pia anajulikana kama Suzzy au Makush na alizaliwa katika mtaa wa mabanda wa Mathare.

“Yeye ndiye kiongozi mwanamke pekee aliyechaguliwa katika Mathare. Wanamwita "Ghetto Girl."

Seneta huyo wa UDA alifichua kuwa ana uhusiano wa karibu na Bi Makungu na kumtaja kama "msichana wangu."

Alitambua kuwa bidii na kujitolea kwa MCA huyo kijana katika kampeni za chama cha Jubilee za 2017 kulimfanya ateuliwe kwenye Bunge la Kaunti ya Nairobi.

"Mkutano wangu wa kwanza na Suzzy ulikuwa katika kampeni za 2017 ambapo alikuwa mhamasishaji mkuu huko Mathare. Suzzy Makungu ni mkarimu lakini mgumu na ni msichana wangu,” Nyamu alisema.

Siku ya Jumanne, Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja alionyesha upande wa hisia ambao haujawahi kushuhudiwa hapo awali alipokuwa akizungumzia mpango wa kulisha watoto shuleni Nairobi.

Wakati akitoa hotuba katika eneo la Roysambu, bosi huyo wa kaunti aliangua kilio alipokuwa akizungumzia mpango wake wa Dishi na County ambao unalenga kuwalisha wanafunzi wa Nairobi.

Akitoa hotuba yake mbele ya Rais William Ruto, Sakaja alisimama kwa muda huku akimwaga machozi, akasimulia jinsi mpango huo ulivyokuwa muhimu kwake.

"Samahani mheshimiwa lakini ni uchungu ya hawa watoto wanakosa chakula," alisema.

Sakaja alimpongeza rais kwa kuunga mkono mpango wake wa kulisha shuleni.

"Vile watu wanakumbuka maziwa ya nyayo watu watakumbuka chakula cha Ruto," alisema.