"Alikuwa shy" Mke wa Stivo akiri ndiye alimtongoza msanii huyo, azungumzia kucheatiwa na Pritty Vishy

“Nilikuwa wa kwanza. Alikuwa shy, mimi sikuogopa kumwambia. Mimi ndiye nilimpea motisha,” Grace alisema.

Muhtasari

•Grace alidokeza kuwa Stivo alikuwa na haya sana kueleza hisia zake na hivyo kumfanya yeye kuwa wa kwanza kuchukua hatua hiyo.

•Grace alifichua kwamba alikuwa kwenye mahusiano na Stivo hata wakati ziliibuka ripoti kuhusu mahusiano yake na Pritty Vishy.

Grace Atieno, Stivo Simole Boy, Pritty Vishy
Image: HISANI

Grace Atieno, mke wa mwimbaji Stivo Simple Boy amefichua kuwa yeye ndiye aliyechukua hatua ya kwanza ya kukiri mapenzi yake kwa msanii huyo kutoka Kibera.

Akizungumza kwenye mahojiano na Vincent Mboya, mrembo huyo kutoka Taita Taveta alidokeza kuwa Stivo alikuwa na haya sana kueleza hisia zake na hivyo kumfanya yeye kuwa wa kwanza kuchukua hatua hiyo.

“Nilikuwa wa kwanza. Alikuwa shy, mimi sikuogopa kumwambia. Mimi ndiye nilimpea motisha,” alisema Grace.

Alisema kwamba mwimbaji huyo wa ‘Mihadarati’ alifurahi sana baada ya yeye kukiri hisia zake hivi kwamba alienda kushiriki habari hizo njema na familia yake.

“Alijisikia vizuri.Hata hivyo hakuniambia. Aliambia watu wa kwao nikakuja kuskiza kwao,” alisema.

Grace alifichua kuwa alikutana na mwanamuziki huyo kwa mara ya kwanza miaka kadhaa iliyopita na wakawa marafiki kabla ya hadithi yao ya mapenzi kuanza.

“Tulikutana Made in Kibra. Nilikuwa nikidensi. Kuna kijana tulikuwa tukidensi na yeye. Yeye ndiye alituunganisha. Kuna wimbo alikuwa akitoka ‘Mihadarati’. Nikaona siwezi na densi walizokuwa wakicheza. Baadaye akaja kutoa I lift you Higher. Hapo ndipo tukajuana na yeye mpaka sasa hivi, namshukuru Mungu,” alisema..

Alifichua kwamba alikuwa kwenye mahusiano na Stivo hata wakati ziliibuka ripoti kuhusu mahusiano yake na Pritty Vishy.

Hata hivyo, anasisitiza kuwa mumewe hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtengeneza maudhui huyo mwenye umri wa miaka 22.

“Akiwa na yeye (Pritty Vishy) bado tulikuwa pamoja. Hata kama Stivo alikuwa ananificha mimi nilikuwa najua kila kitu kuhusu anavyoendelea kimapenzi. Hakuwa ananicheat, aliogopa tu kuniambia. Sidhani yeye na huyo msichana walikuwa na mapenzi," alisema.

Grace ameweka wazi kuwa hakuchagua kuchumbiana na msanii huyo kutoka Kibera kwa sababu ya umaarufu wake bali alifanya hivyo ili kumsaidia kufanikiwa.

Alibainisha kuwa alimtia motisha sana alipokuwa kwenye hatihati ya kuacha muziki kwa sababu ya kutusiwa mitandaoni.

“Sikujua ningeweza kufika na yeye mahali tumefika sasa hivi. Kuna wakati alitaka kupoteza na muziki. Watu walikuwa wakimtusi kutokana na jinsi anakaa. Mimi ndiye nilikuwa namtia moyo asipoteze matumaini aendelee tu,” Grace alisimulia.

Aliongeza, “Aliniongelesha na mamake na dada zake wakasema ndivyo namsapoti basi itabidi akae na mimi. Kwetu sio wengi wanampenda lakini mapenzi...”

Stivo alimtambulisha Grace kama mke wake hadharani wakati wa mazishi ya babake mapema mwaka huu.