"Fear women!" Gidi alalamika baada ya kupotoshwa na mwelekezi mwanamke wa Google Maps

Mtangazaji Gidi Ogidi amekuwa akifurahia wakati wake kijijini.

Muhtasari

•Siku ya Jumamosi, mtangazaji huyo tajika alisimulia jinsi Ramani za Google zinaweza kumfanya mtu apotee kijijini.

•Gidi alielezea kusikitishwa kwake na ramani za google kupotosha mtu kisha hatimaye kujipatia sifa baada ya kuhangaika kuomba maelekezo.

Mtangazaji Gidi Ogidi

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi kwenye Radio Jambo, Joseph Ogidi almaarufu Gidi Ogidi amekuwa akifurahia wakati wake kijijini.

Gidi amekuwa akirekodi na kushiriki matukio yake mengi ya kufurahisha kijijini na mashabiki wake kupitia akaunti zake rasmi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Siku ya Jumamosi, mtangazaji huyo tajika alisimulia jinsi Ramani za Google zinaweza kumfanya mtu apotee kijijini.

““Huku village unaweka google maps inakupoteza then unauliza locals wanakupatia maelekezo halisi. Ukiwa njiani huyo mama wa Googles anawika eti turn right, make a u turn, make a u turn now, make a u turn please,” Gidi alisimulia.

Aliendelea, “Sahizo wewe unapambana tu na maelekezo umepewa na mtu wa Bodaboda. Kidogo kidogo unafika mahali ulikuwa unaenda, alafu huyo mama wa google maps anasema  ati …’You have arrived at your destination.(Umefika mahali ulikuwa unaenda).”

Mwanamuziki wa zamani wa kundi la Gidi Gidi Maji Maji alielezea kusikitishwa kwake na ramani za google kupotosha mtu kisha hatimaye kujipatia sifa baada ya kuhangaika kuomba maelekezo.

“Yaani baada ya kuhangaika peke yangu kutafuta eneo hili bado unadai credit? Haki fear women (waogope wanawake)!,” alisema.

Je, umepitia yapi kibinafsi na ramani za google? Shiriki nasi kwenye majukwaa yetu mbalimbali ya mitandao ya kijamii.

Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, mtangazaji Gidi amekuwa hayupo hewani kwa likizo fupi na anatarajiwa kurejea wiki inayokuja.

Mtangazaji mwenzake Jacob Ghost Mulee amekuwa akiendesha kipindi hicho vizuri wakati Gidi alipokuwa hayupo na mashabiki wa Gidi na Ghost Asubuhi watafurahi sana kuwasikia watangazaji hao wawili mahiri wamerudi pamoja.

Usikose kipindi chako unachokipenda cha Gidi na Ghost kesho, Jumatatu kuanzia saa kumi na mbili hadi saa nne kamili asubuhi.