Akothee ajibu madai ya kuiba mume wa mwanamke mwingine, afichua jina la mtoto aliyempoteza

"Kwani ni handbag, huyo aliibiwa umemuona kwa hiyo love story?” Akothee alijibu.

Muhtasari

•Wanandoa hao walikutana mjini Zurich, Uswizi mnamo Julai 16, 2022 na kuanza safari yao ya mapenzi kabla ya kufunga ndoa Mei mwaka huu.

•Akothee alizungumzia kuhusu kupoteza ujauzito wake na Omosh mwishoni mwa mwaka jana, mizozo ya kifamilia na masaibu mengine ambayo walijipatana wakikabiliana nayo.

wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Akothee na mumewe Denis Shweizer wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Siku ya Jumapili, Julai 16, mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee na mumewe Denis Shweizer waliadhimisha mwaka mmoja wa uchumba.

Wanandoa hao walikutana mjini Zurich, Uswizi mnamo Julai 16, 2022 na kuanza safari yao ya mapenzi kabla ya kufunga ndoa Mei mwaka huu.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, mama huyo wa watoto watano alifichua kuwa mume huyo wake mzungu alimvisha pete ya uchumba katika mkutano wao wa tatu na baada ya hapo akamtambulisha kwa wazazi wake nchini Italia.

"Mnamo tarehe 16 Julai 2022, nilikutana na mume wangu nchini Uswizi mji wa Zurich kwenye ziwa la Zug. Mnamo tarehe 18 Julai 2022 tulikuwa na kikao cha pili katika jiji la Bern kwenye bahari ya Murten. Hakuniruhusu nirudi kwenye makazi yangu.. Tulikwamiliana kama gundi , Alinisindikiza hadi Ujerumani Dusseldorf ambapo shoo yangu ilikatizwa. Promota alikataa kulipa salio la show kwa sababu nilijitokeza na mwanaumena alitarajia kuniona peke yangu kwa hiyo sikupiga shoo hata hivyo ilikuwa imeuzwa..Mkutano wetu wa tatu ulikuwa milimani, Denis Omondi aliniharibu na mahaba.. Nilijisahau na akanifagia kutoka kwenye miguu yangu. Kisha akanichumbia na kuniuliza kama anaweza kunitambulisha kwa familia yake. Nikasema ndio nipo tayari. Kisha tuliendesha gari hadi Italia na katika siku ya kuzaliwa ya mama yake, alijivunia kumtambulisha mke wake mtarajiwa," Akothee alisimulia.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 aliwasifu wakwe zake na kufichua kuwa wao ni familia ya kibinafsi ambayo haiko kwenye mitandao ya kijamii.

Pia alifichua kuwa mipango ya harusi yake na mzungu huyo ilianza mwezi Septemba mwaka jana wakati alipozuru Kenya.

“Ilitakiwa kuwa NYOMBO lakini mambo husambaratika. Tulikuwa na mabadiliko mengi, ya ukumbi, mada bla bla. Haikuwa rahisi kwani ilikuwa ni mshtuko kwa kila mtu. Jina la OMOSH lilinitoka mimi, ninavutiwa na utaratibu wa mume wangu wa asubuhi na jinsi anavyofanya mambo yake, Omondi ndiye mwanaume ambaye nimekuwa nikitamani kuwa naye siku zote, ni toleo langu la kiume linapokuja suala la kazi,” alisema.

Akothee pia alizungumzia kuhusu kupoteza ujauzito wake na Omosh mwishoni mwa mwaka jana, mizozo ya kifamilia na masaibu mengine ambayo walijipatana wakikabiliana nayo.

“Mnamo Novemba 4, 2022 tulitangazwa kuwa wajawazito, safari ya kulea mtoto ikaanza, Bw Omosh alimwita mtoto wake Esedua. Omosh alirudi nchini kwao ili kutangaza habari kwa familia yake na alirudi tarehe 16 Desemba 2022. Tarehe 17 Desemba tulipoteza mimba, Siku hiyo hiyo, nguruwe wake walizaliwa. Tulikuwa na mengi ya kukabiliana nayo mbali na kamera . Migogoro ya kifamilia kutoka upande wangu, biashara, uhusiano, harusi ijayo, kufiwa na mtoto wetu mchanga na visa vya kusisimua mtandaoni, blogu na hadithi ghushi,” Akothee alisimulia.

Kufuatia taarifa yake ya kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja, alilazimika pia kuzungumzia madai ya kumpokonya mumewe kutoka kwa mwanamke mwingine baada ya mwanamitandao kumshutumu.

"Heri ya kumbukumbu ya mwaka, vipi kuhusu uvumi kwamba umemuiba mpenzi??" shabiki aliuliza.

Alijibu, "Umesema tayari ni uvumi, unataka jibu gani? Kwani ni handbag, huyo aliibiwa umemuona kwa hiyo love story?”