"Kutoka injili hadi porn!" Hisia mseto baada ya Bahati na mkewe Diana Marua kuigiza kitandani

Katika video hiyo, Bahati alionekana kupendekeza tendo la ndoa huku mkewe Diana Marua akiwa amelala naye.

Muhtasari

•Bahati alionekana akimsumbua Diana Marua wakati akiwa amelala, hatua iliyomfanya mama huyo wa watoto watatu kuamka.

•Baadhi ya wanamitandao walionekana kufurahia video hiyo, baadhi waliikosoa huku wengine wakionekana kuwahukumu wanandoa hao kuhusu maudhui ya video hiyo.

Diana Marua na mumewe Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Siku ya Jumatatu, mwimbaji wa zamani wa nyimbo za injili Kelvin Kioko almaarufu Bahati alichapisha video ya burudani ambayo aliigiza na mkewe Diana Marua  kitandani.

Katika video hiyo, Bahati alionekana akimsumbua Diana Marua wakati akiwa amelala, hatua iliyomfanya mama huyo wa watoto watatu kuamka.

"POV: Unaamka na kupata kitu kinachokushtua saa nane usiku," yalisomeka maelezo mafupi yaliyoandikwa kwenye video hiyo.

Katika video hiyo, mwimbaji huyo alionekana kutoa mapendekezo ya tendo la ndoa huku mkewe akiwa amelala naye.

Baada ya kuamka, Diana alionekana kutuliza kiungo cha mumewe huku akisema "Wewe ni kijana mbaya" kabla ya kuendelea kulala.

“Mimi ni Kijana Mbaya au Kijana Jasiri?? Bahati aliwauliza mashabiki wake chini ya video hiyo aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kama kawaida, watumiaji wa mtandao walikuwa wepesi kutoa maoni yao mbalimbali kuhusu maudhui ya chapisho hilo.

Baadhi ya wanamitandao walionekana kufurahia video hiyo, baadhi waliikosoa huku wengine wakionekana kuwahukumu wanandoa hao kuhusu maudhui ya video hiyo.

Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao Wakenya:-

skiddybwoy: From gospel to p#rn star.. sad generations ina lost.

nicki_bigfish: Heaven na Majesty wanyan'anywe simu at this rate.

ladyzmali: Your reputation will either make your children rejected/frowned upon or make them accepted when you are no more. "A good name is to be desired more than expensive perfume."

chirrie: Another reason why parents should not give kids who are 13 years and below phones. This is soft porn. This is how they get introduced.

_itsgracemutula_ stop the hate.. marriage is meant to be enjoyed. Pata mpoa wako mfanye hivi pia.

young_poetry_niccu254 Na hivyo ndio ukasahau story na gospel.