"Chorea kwanza!" Bahati akataa ofa ya mkewe Diana Marua ya kumzalia mtoto wa nne

Diana alidokeza kwamba kwa jinsi anavyompenda sana mwanamuziki huyo, yuko tayari hata kumzalia mtoto wa nne.

Muhtasari

•Diana alimsifu Bahati kwa mapenzi yake kwake na kufunguka sababu kadhaa zilizomfanya achague kuwa na mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili.

•Bahati alidokeza kwamba hata kama ofa ya mke wake kumzalia mtoto mwingine ilikuwa tamu; hayuko tayari kwa mtoto mwingine.

Diana Marua na mumewe Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Siku ya Jumapili, mwanavlogu mashuhuri Diana Marua alizamia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo aliandika ujumbe mrefu mzuri kwa mumewe Bahati.

Katika chapisho lake, mama huyo wa watoto watatu alimsifu Bahati kwa mapenzi yake kwake na kufunguka sababu kadhaa zilizomfanya achague kuwa na mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili.

Diana alimtaja mumewe kuwa mtu anayemuelewa na akadokeza kuwa mzazi huyo mwenzake alimkubali kuwa mke wake pamoja na dosari zake zote. Wakati huo huo, alidokeza kwamba kwa jinsi anavyompenda sana mwanamuziki huyo, yuko tayari hata kumzalia mtoto wa nne.

“Huyu mtu hapa Bahati. Kusema kweli nitakubebea mtoto mwingine, Mungu akipenda. Mume wangu, Mfalme wangu, Rafiki yangu wa karibu, Msiri wangu, Mpenzi wangu wa Umbea, Dawa yangu, anayenielewa kuliko ninavyojielewa, Babe, niruhusu kukufungulia moyo wangu,” Diana aliandika kwenye Instagram.

Aliongeza, "Kila wakati ukinikumbusha tulikotoka, tunaishia kucheka juu yake, kulia au kufurahiya tu kwamba hatukukata tamaa. Nilitulia na wewe kwa sababu nilitaka mtu anipende pamoja na dosari zangu zote na nilipokutana na kujumuika na wewe, ulikuwa tofauti. Nilipenda jinsi ulivyozungumza nami. Ilikuwa kweli.”

Rapa huyo aliambatanisha ujumbe wake na picha za mwimbaji huyo wa kibao cha ‘Mama’.

Aliendelea kusherehekea safari yao ya mapenzi ya miaka saba huku akifichua kuwa haikuwa rahisi kwani wametengana na kurudi tena takriban mara saba.

Hata hivyo alidokeza kuwa mara ambazo amewahi kutengana na mwanamuziki huyo zimegeuka kuwa masomo ambayo yamewafanya kuwa bora kwa kila mmoja.

"Kuachana kulitufanya kutambua kwamba tunaweza kutofautiana kwa sababu sisi ni tofauti lakini haikumaanisha tupendane kidogo. Daima unachagua kuwa mtu mkubwa zaidi na kusimama kidete kwa upendo wetu. Umenifunza kuwa mapenzi ni subira, kusamehe, fadhili na upendo hunishika usiku hata wakati nimekukasirisha,” alisema.

Mama huyo wa watoto watatu pia alichukua fursa hiyo kumuahidi mumewe mapenzi na utegemezo mwingi wanapoendelea kusitawisha ndoa yao.

Katika jibu lake, Bahati alidokeza kwamba hata kama ofa ya mke wake kumzalia mtoto mwingine ilikuwa tamu; hayuko tayari kwa mtoto mwingine.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hata hivyo alimhakikishia mkewe kuwa anampenda sana na kusema amebarikiwa kuwa naye.

“Sweetheart hapo Kwa mtoto nwingine Chorea Kwanza. Lakini juu ya yote naamini kwa kujiamini wewe ni mfupa wangu uliokuwa unakosekana... Mara kwa Mara Nitakuita Msichana Wangu Wa Ndoto Mwanamke Kila Mwanamke Angetamani Kumwita Wifey... Nimebarikiwa Kukuita Wangu. Nitakupenda mpaka Enternity,” Bahati alisema.