Mpenzi wa Crazy Kennar atoa taarifa ya huzuni kuhusu kifo cha mtoto wao

Bi Natalie Asewe amekiri kukumbwa na majonzi sana katika kumuomboleza marehemu mtoto wao.

Muhtasari

•Mnamo Desemba 16, wakati wa shoo yake ya ‘Happy Country’, Crazy Kennar alisema mwanawe aliaga siku nne kabla ya siku hiyo.

•"Simuombolezi tu mwanangu, ninaomboleza kutopata nafasi kamwe ya kumsikia akilia, kumsikia akizungumza, kumfundisha kutembea na kumuona akikua," Natalie alisema.

na mpenzi wake Natalie Asewe
Crazy Kennar na mpenzi wake Natalie Asewe
Image: HISANI

Siku chache baada ya mchekeshaji Crazy Kennar kufichua  kwamba alipoteza mtoto wake kabla hajazaliwa, mpenzi wake pia amefunguka kuhusu msiba uliowakumba..

Mnamo Desemba 16, wakati wa shoo yake ya ‘Happy Country’ iliyofanyika katika KICC, Crazy Kennar alisema mwanawe aliaga siku nne kabla ya siku hiyo..

“Kwa bahati mbaya, mwanangu alifariki siku nne zilizopita. Kwa hiyo imekuwa safari ngumu sana kwangu kwa sababu tulilazimika kupitia hayo na wakati huo huo kufanya shoo," alisema.

Mpenziwe Crazy Kennar, Natalie Asewe kwenye ukurasa wake wa Instagram  alikiri kukumbwa na majonzi sana katika kumuomboleza marehemu mtoto wao.

"Wanasema hakuna uchungu mkubwa kuliko kuzaa, lakini sikubaliani. Maumivu makubwa zaidi duniani ni kubeba na kuzaa mtoto ambaye hutawahi kumlea."

Huku akionyesha picha yake ya wakati alipokuwa mjamzito sana, Natalie aliongeza;

"Simuombolezi tu mwanangu, ninaomboleza kutopata nafasi kamwe ya kumsikia akilia, kumsikia akizungumza, kumfundisha kutembea na kumuona akikua."

Kila siku mpya inaonyesha kitu ambacho atakosa. Ulikuwa mkamilifu kwa kila njia. Malaika katika Kitabu cha Uzima aliandika kuzaliwa kwa mtoto wangu, kisha akanong'ona alipokuwa akifunga kitabu, 'Ni mzuri sana kwa dunia hii.'

Mtayarishaji wa maudhui Stanley Omondi ambaye alikuwa sehemu ya wafanyakazi wa Crazy Kennar alimhakikishia kuendelea kumsapoti wanapoomboleza.

"....Maumivu ni mazito lakini Pamoja tunasimama," aliandika.

Soma maoni mengine ya kumfariji Natalie hapa chini;

bettypeters1 Hugs sweety, Bwana mwema akufariji na kukuweka imara,Hakika atakurudishia maradufu. ������❤️❤️

austin_muigai Mungu akufariji katika nyakati hizi❤️

k.i.b.z._ Uko vizuri Natalie,.Mungu atakusimamia

theetall_hype_savage Sending nothing but love your way... sijui inajisikiaje na siwezi hata kufikiria... Pole za dhati kwako @crazy_kennar and fam.. Mungu awatie nguvu