Wimbo mpya wa msanii Nay wa Mitego kutoka Tanzania 'Wapi Uko' wazua mjadala Kenya

Wimbo huo unaangazia taifa` fulani linaloandamwa na uongozi mbovu, rushwa, njaa na ukosefu wa fursa za ajira kwa vijana wake

Muhtasari

•Wakenya wameachwa vinywa wazi kufuatia wimbo wa rapa kutoka Tanzania Nay wa Mitego, uliozungumzia kuhusu nchi isiyojulikana.

•Wimbo huo kufikia sasa umeibua mjadala kwenye Twitter, huku Wakenya wakitofautiana iwapo mwimbaji huyo anawalenga.

Msaani Ney wa Mitego
Msaani Ney wa Mitego
Image: BBC

Wakenya wameachwa vinywa wazi kufuatia wimbo wa rapa kutoka Tanzania, Emmanuel Elibariki, maarufu Nay wa Mitego, uliozungumzia kuhusu nchi isiyojulikana.

Wimbo huo wa “Wapi huko” unaangazia taifa` fulani linaloandamwa na uongozi mbovu, rushwa, njaa na ukosefu wa fursa za ajira kwa vijana wake.

Katika wimbo huo, Nay anasimulia jinsi nchi inavyoonekana kuwa nzuri na yenye mafanikio mbele ya ulimwengu, lakini watu wake wanateseka chini ya viongozi wazembe, vijana wake wanasota kwenye umasikini na wasichana wake sasa wameingia kwenye pesa kuliko mapenzi.

Zaidi ya hayo, rapa huyo anawachana vijana kwa kuwatafuta akina kina mama wenye fedha, kuzungumza Kiingereza kizuri na kujigamba jinsi nchi yao ilivyo bora kuliko majirani zao, lakini nyumbani kwao hawana hata umeme.

Wimbo huo kufikia sasa umeibua mjadala kwenye Twitter, huku Wakenya wakitofautiana iwapo mwimbaji huyo anawalenga, au anaangazia tu matatizo yanayoikumba nchi yake.

Conrad Kulo mmoja alisema: "Tanzania inatupika kihalisi. Jirani hana unga, hana umeme, ni kingereza tu slur sasa imepikwa studio, na niwaambie Maina, William Ruto lazima aende.

"Hata hivyo, mtumiaji wa X Mwabili Mwagodi alitofautiana naye akisema Nay analenga tu uongozi wa Tanzania.

"Ni mambo ambayo Wakenya hawajaelewa kabisa kwamba Ney wa Mitego anakejeli uongozi wa Tanzania kwa kuibeza Kenya bado Tanzania ndiyo imeingia shimoni.

Mwanamume anayejiita jina la Elon’s Musk anasema kwamba siamini msanii wa Tanzania ndiye anayeweza kuja kuelezea shida zilizopo Kenya kwasababu wasanii wa Kenya wana mambo mengi kichwani