Josh Wonder afichua maisha yake ya mapenzi na mambo mengine

Watu wanasema kuwa mpenzi wake anafanana na ex wake lakini kulingana na yeye ni watu wawili tofauti.

Muhtasari
  • Katika mahojiano yake na Oga Obinna alieleza  kuwa hayuko single ingawa hakufichua jina ya mpenzi wake.
  • Mtandao kulikuwa na mjadala kuwa ako na uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa ex wake lakini hajaeleza ukweli wa mambo hayo.

Josh Wonder
Image: Instagram

Mkuza Maudhui Joshua Angachi  almaarufu Josh Wonder amefunguka kuhusu maisha yake ya mapenzi na mambo mengine kumhusu.

Katika mahojiano yake na Oga Obinna alieleza  kuwa hayuko single ingawa hakufichua jina ya mpenzi wake.

"Siko single, niko kwa mahusiano ya kimapenzi na mtu".

Aliendelea kusema kuwa watu wanasema kuwa mpenzi wake anafanana na ex wake lakini kulingana na yeye ni watu wawili tofauti.

Mtandaoni kulikuwa na mjadala kuwa ako na uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa ex wake lakini hajaeleza ukweli wa mambo hayo.

Amefichua pia kuwa alisomea shule ya sekondari ya Butere Boys na alipate alama ya A- na baada ya hapo alienda chuo kikuu cha JKUAT kufanya sayansi ya kompyuta ambapo alisoma kwa mwaka mmoja kisha akaenda chuo kikuu cha Daystar ambapo anasomea taaluma ya uanahabari akiwa katika mwaka wake wa mwisho.

"Mimi ni mwanachuo wa Butere Boys. Nilipata A lakini  ilikuwa na minus so ni A-". 

"Kutoka sekondari nilienda JKUAT Kwa mwaka mmoja alafu nikaenda Daystar na niko mwaka wangu wa mwisho huko"

Aliendelea kueleza kuwa waundaji maudhui Sean mmg na Flirty Carlos walimsaidia sana kusimama tena wakati alikuwa katika hali mbaya zaidi.

"Flirty Carlos na Sean mmg ni mandugu zangu sana.  Urafiki wetu ni wa binafsi zaidi kuliko venye watu waniona huku nje. Hao ni walionishikilia mkono wakati nilikuwa hali mbaya zaidi."

Alifichua kwamba alshaendelea na maisha yake lakini bado anamkosa sana ex wake.

"Nilishapoa kitambo sana lakini  kumkosa ex wake ni jambo la kawaida".