Hisia mseto baada ya Director Trevor kumtangaza mrithi wa Eve Mungai

Trevor alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akisema kuwa Eve Nyaga atachukua nafasi ya Eve Mungai.

Muhtasari
  • Trevor amemtambulisha Eve Nyaga kama sura mpya ya chaneli yake ya YouTube baada ya mshirika wake wa zamani, Eve Mungai kuondoka.
Director Trevor na Eve Nyaga
Image: Instagram

Director Trevor amemtambulisha Eve Nyaga kama sura mpya ya chaneli yake ya YouTube baada ya mshirika wake wa zamani, Eve Mungai kuondoka.

Mnamo Machi 18, 2024, Trevor alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akisema kuwa Eve Nyaga atachukua nafasi ya Eve Mungai.

Trevor alichapisha picha zake kadhaa akiwa na Eve Nyaga kwenye mitandao ya kijamii.

"Tunawaletea sura mpya zaidi ya Kenya Online Media, mtangazaji wetu mahiri na taswira ya chapa Eve Nyaga! Jitayarishe kuzama katika kiini cha burudani Eve anapokuletea miiko ya kipekee na kufafanua hadithi zilizo nyuma ya vichwa vya habari. Kaa tayari kwa safari iliyojaa msisimko, maarifa, na burudani isiyo na kikomo anapoleta shauku na ustadi wake mbele!"Trevor aliandika.

Kuzinduliwa kwa mtangazaji mpya kumeibua maoni mseto kutoka kwa wanamitandao.Tazama  baadhi yao;

shes_kemunto: Eve🔥🔥🔥🔥🔥congratulations bossy

wa_kina_fellow: Ama wewe ni Adam 😂😂 lazima utafute Eve

2mbili:EVEntually Huyu AtawakaNYAGA Wote!

davidoofficialke:Bro msipendane kwanza please 😢

mrbradely_: Mungai Eve ❌️ Nyaga Eve✅️😂😂

hon.antonymanyara:Why Eve, mkuu? But then nmekumbuka mambo ya Adam & Eve. Viva!

bien._son:Director Adam😂😂

2mbili:Congrats Broo ❤️! Keep Winnning

pireeh_: this whole documentary<<<<<<<<<

king.kalala:Nilijua Adam si fala😂

Katika mfululizo wa instastorie, Trevor alifichua kwamba alikuwa amechukua udhibiti kamili wa chaneli ya YouTube na hakuhitaji tena huduma za Eve Mungai.