Hisia mseto baada ya mwimbaji Christina Shusho kufichua sababu ya kugura ndoa yake

Licha ya uamuzi muhimu wa kuondoka nyumbani, Shusho alisisitiza kuwa mchakato huo ulikuwa wa amani.

Muhtasari
  • Alifichua kwamba uamuzi wake wa kuondoka ulitokana na ndoto aliyoota, ambayo aliamini kuwa ni mgawo wa kimungu aliohitaji kutekeleza kwa moyo wote.
Christina Shusho
Christina Shusho
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa Tanzania Christina Shusho ameangazia uamuzi wake wa kuondoka kwenye nyumba yake ya ndoa, akitaja haja ya kuzingatia wito wake.

Katika mahojiano na New Jerusalem Church TV, msanii huyo mashuhuri alizungumzia ufahamu kuhusu safari yake na sababu za yeye kuondoka nyumbani kwake.

Alifichua kwamba uamuzi wake wa kuondoka ulitokana na ndoto aliyoota, ambayo aliamini kuwa ni mgawo wa Kimungu aliohitaji kutekeleza kwa moyo wote.

"Kwa ajili yangu, acha niongee tu roho safi. naomba watakaofuatilia na wafuatilie na waamini huyu ndio mimi. Sijawahi kuwa bandia, na sisemi uwongo. Ukweli ni kwamba, ni kazi tu. Hakuna tofauti zaidi ya hiyo. Kazi ambayo Mungu amenipa msimu huu haiwezi kuniruhusu kubaki pale nilipokuwa. Ilinibidi niondoke ili nitimize kazi,” alisema.

Licha ya uamuzi muhimu wa kuondoka nyumbani, Shusho alisisitiza kuwa mchakato huo ulikuwa wa amani. Alisimulia jinsi alivyomwendea mume wake kwa heshima na kumwomba usaidizi wa kumwachilia aanze safari yake.

"Nilimwambia aniruhusu kubeba mzigo wangu kama kawaida. Acha nibebe mzigo wangu, na wewe uendelee na huduma yako. Hakukuwa na shida kabisa," alisema, akisisitiza maelewano kati yao.

Alifafanua kuwa wakati wakiwa wameunganishwa katika ndoa, wito wao ulikuwa tofauti na alielezea umuhimu wa kuheshimu njia za kipekee za kila mmoja na kufikia makubaliano kwa kuzingatia maelewano.

Kufuatia ufichuzi wake, kauli za Shusho zilizua hisia tofauti mtandaoni. Ingawa wengine walitilia shaka ulazima wa kuondoka nyumbani kwake ili kutimiza huduma yake, wengine walionyesha kumuunga mkono na kumtakia heri safari yake mbeleni.

Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mtandao;

MmoⓂ️: Ni assignment tu, meaning they separated,just simple..asieleze sana,

Cubby: i understand what she means.. haya maisha hayaitaj unafk.. you do you Ms shusho

Magreth J Lakath: very true ✍️

Favour🇹🇿: No assignment given by God will remove you from an institution He God Himself has blessed..

VM: kuna mwanaume akikuoa hataki uendelee anataka akutawale kila kitu mwacheni awe huru

M Situmah: hapa kuna kitu shusho hatuambii..