"Sijui la kufanya kwa wakati huu!" Mr Seed azungumzia kumpoteza mama yake

Mzazi huyo wa Mr Seed alikata roho mwezi uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Muhtasari

•Siku ya Jumanne jioni, mwimbaji huyo alichapisha picha nzuri ya mama yake na chini yake akafunguka jinsi anavyom’miss marehemu.

•Mr Seed alitangaza kifo cha mama yake mpendwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mr Seed na marehemu mamake
Mr Seed na marehemu mamake

Mwimbaji wa nyimbo za injili na za mapenzi Moses Tarus Omondi almaarufu Mr Seed ameendelea kuomboleza kufuatia kifo cha mama yake.

Mzazi huyo wa Mr Seed alikata roho mwezi uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu. Hii imemuacha msanii huyo katika hali ambayo hajui jinsi ya kukabiliana na msiba huo.

Siku ya Jumanne jioni, mwimbaji huyo alichapisha picha nzuri ya mama yake na chini yake akafunguka jinsi anavyom’miss marehemu.

"Nitakukosa ma... sijui la kufanya kwa wakati huu," Bw Seed alisema.

Mr Seed alitangaza kifo cha mama yake mpendwa mwishoni mwa mwezi uliopita, siku chache baada ya kuwataka mashabiki wamuombee.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi alizamia kwenye mitandao ya kijamii kutangaza kifo cha mzazi huyo wake katika ujumbe mfupi uliosomeka;

"Pumzika sasa mpenzi wangu 💔💔 nitakupenda milele 🧡🧡." Mr Seed aliandika.

Katika ujumbe wa kihisia-moyo wiki iliyotangulia, Bw Seed alisema mamake alikuwa akiingia na kutoka hospitalini.

"Nimekuwa nikiingia na kutoka katika hospitali mbalimbali kwa muda wa mwaka 1 na nusu nikijaribu kutafutia mama yangu matibabu.. inasikitisha sana kuona mama yetu akiteseka kila siku 💔💔 .. lakini bado Mungu ni mwaminifu na tunamtumaini na kumuombea apone. .. sasa hivi amelazwa The Luton Hospital wanamhudumia vyema, wauguzi na madaktari wote wanaofanya kazi usiku na mchana Mungu awabariki,” alisema.

Aliwashukuru madaktari waliokuwa wakimhudumia mama yake.