
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sidika alichapisha picha
akiwa amestarehe kwenye ndege na kufichua kuwa ndio alikuwa anarudi nchini
Kenya baada ya ziara ya siku kadhaa nchini Marekani.
Kwa mujibu wa Sidika, anatarajia kufanya ziara moja ya
kimataifa nje ya Kenya angalau mara moja kwa mwezi, akifichua tayari mwezi
Februari amekamilisha safari 2 kimataifa.
Mama huyo wa watoto wawili aliwapa ushauri wa bila malipo
mashabiki na wafuasi wake akiwaasa kwamba ikiwa wangependa kuishi maisha ya
afya bila kulazimika kuonana na daktari mara kwa mara, basi wafanye kuwa
kawaida kwao kusafiri nje ya nchi angalau mara moja kwa mwezi.
“Narejea kwenye uhalisia
…Narudi Kenya 🇰🇪✈️ Kwa kweli nilipata
msisimko 💥 hakika safari 1 ya
kimataifa kwa mwezi huwaweka madaktari mbali! Ni Mwezi wa 2; na tayari
nimekamilisha ziara kwa nchi 2. Siwezi kusubiri matukio ya Machi,” Sidika alikariri.
Watu katika kutoa maoni walimshabiki kwa kile walidai kwamba
yeye ndiye mwanasosholaiti asiyeogopa kumtumia esa kujivinjari.
Wengine walijisikitikia kwamba hana kaunti za Kenya 47
hawajawahi zizuru zote wakati Sidika tayari analeta wazo la kusafiri kimataifa
angalau mara moja kwa mwezi.
@simba.tito: “Mimi mwenyewe 47 counties sijamaliza.”
@bellah_ayuma: “God, please, futa hio yenye nlikua nmesema
when I grow up, I want to be Amberray futa ueke Vera please.”
@doriceliyoko: “Ukianza kucatch flights hutaki kamwe kuacha
aki. Ni kama dawa.”
Ungamo la Sidika kuhusu kuwa na uraibu wa kusafiri kimataifa angalau mara moja kwa mwezi linajiri wakati ambapo nchini kumekuwa na vita vya maneno baina ya mwanasosholaiti Amber Ray na baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii.
Mgogoro huo ulianza pale ambapo baadhi walimsuta Amber Ray wakimtaka kukoma kujitambua kama 'bibi ya tajiri' wakati hajawahi fanya ziara ya nje ya nchi.
Hata hivyo, Amber Ray alijitetea akionesha risiti za ziara zake za nje ya nchi, risiti ambazo zilichambuliwa vikali na kudhihakiwa.