
VERA Sidika ametetea wanaume kutoka jamii yake ya Abaluhya akisema kuwa hao ndio wanaopenda wanawake wenye viuno vipana.
Akizungumza na mwanablogu Afolasade Samagbeyi kupitia kwa
podkasti yake, Sosholaiti huyo alisema kuwa wanaume Waluhya si tu wanapenda
wanawake waliobarikiwa na upana wa viuno lakini pia wanajua jinsi ya
kuwadekeza.
Sidika alikuwa anajibu swali la Samagbeyi aliyetania kwamba
angependa kuolewa na mwanamume wa Kenya lakini akawa hajui ni wanaume wepi wa
Kenya ambao wanaweza kumpenda jinsi alivyo.
Vera Sidika akirejelea umbo la kiuno kipana cha Samagbeyi,
alisema kwamba wanaume wa Kenya wengi wao wanapenda wanawake wenye wako na ‘curves’
lakini akawapigia upato zaidi wanaume Waluhya akisema ndio wanajua ku’treat
wanawake curvy vizuri.
“Wanaume wa Kenya huwa
wanapenda curves lakini ninafikiria ni nani atakuweza…. Lakini nahisi wanaume
Waluhya – jamii yangu hiyo – wanakuweza sana.”
“Nahisi Waluhya wako
zaidi kama Wanigeria., unajua wana miili yenye nguvu na wanavutia na unajua
wako na vibes nzuri na pia wanajua kudekeza. Utapenda na utakuwa unapika ugali…kwa
kweli siwezi ngoja,” Sidika alimtania Samagbeyi.
Hii si mara ya kwanza kwa mama huyo wa watoto wawili kufichua
waziwazi mapenzi yake kwa wanaume Wanigeria.
Mwezi Mei mwaka jana, Sidika alifichua kwamba alikuwa katika
mahusiano ya kimapenzi na mwanaume kutoka Nigeria, japo akasisitiza kwamba huba
lao si la kuelekea katika ndoa bali ni kujivinjari tu.
"Kwangu mimi, sitaki
kujitolea chochote kwa sasa. Nataka tu kufurahia – niko na mtu lakini sitasema
niko kwenye uhusiano wa dhati. Ni kama sijajitolea kwa sababu sikutaka iwe
serious...niko 50/50 mguu mmoja ndani, mguu mmoja nje.”
"Sitaki ajitume na
sitaki kujitolea. Yeye ni Mnigeria. Unajua jinsi wanavyosema ukiwa mweusi
haurudi nyuma, ni kama ukienda Nigeria haurudi nyuma. Ilikuwa kama nilipotea
mahali fulani na sasa nimerudi kwa mtu sahihi,” alisema.
Vera alizidi kusema kuwa; "Wanaume wa Nigeria wanapenda
wanawake walio na viuno pana…Wanaume wa Nigeria ni wanaume sana na hawaogopi
mtu yeyote, hawaogopi kukuambia unapokosea na ninahitaji hilo.”