
SOSHOLAITI Vera Sidika amefichua baadhi ya dhana potovu ambazo watu wanazo dhidi yake, haswa kuhusu urembo.
Akizungumza kwenye podikasti ya mwanablogu wa Nigeria
Afolasade Samagbeyi, Sidika alifichua kwamba idadi kubwa ya watu wanadhani
kwamba hana lingine lolote la kutoa zaidi ya kiuno chake kipana.
Mama huyo wa watoto 2 alisema kwamba watu wengi hudhania
kwamba yeye ni zuzu asiye na akili licha ya kubarikiwa na mwili mzuri lakini
akakanusha akisema kwamba wale ambao wamekutana naye wanamjua kama mtu mwenye
akili nyingi ajabu.
“Watu wanadhani kwamba
ooh Vera ako na kiuno kipana…ni kama hicho ndicho kitu pekee anacho. Watu wengi
kwenye akili zao wanadhani kwamba hicho ndicho kitu pekee ninaweza kuwa nacho.”
“Watu huwa hawafikirii
kwamba kunaweza kuwa na mengi ya ziada kwa huyu mrembo. Watu ambao wako karibu
na mimi ndio wanamjua Vera wa ukweli na hicho ni kitu ambacho siwezi nikasimama
nikimthibitishia kila mtu.”
“Kwa bahati mbaya wengi
wanadhani kwamba mimi nina makalio makubwa bila akili lakini ukweli ni kwamba
mimi ni mahiri sana acha nikwambie,” Vera Sidika alijieleza.
Kuhusu uhalali wa kiuno chake kipana, Vera Sidika alisisitiza
kwamba ni halisi na asili kabisa akisema hujawahi fanya upasuaji hata mara
moja.
“Unadhani niliwahi
kufanya BBL? Hapana! Huu mwili wangu ni asili kabisa. Nahisi kwamba sababu
inayowafanya watu kudhani kwamba nilifanya BBL ni kutokana na kuna wakati
nilifanya picha ya utani mitandaoni ambayo nilihariri na kukata kabisa makalio
yangu nikidanganya kwamba nilipatwa na dharura ya kimatibabu.”
“Mwili wangu ni asili
kabisa na hata unaweza gusa,” aliongeza.
Mrembo huyo alisema kwamba jambo kuu analojivunia zaidi
katika maisha yake mpaka sasa ni uamuzi wa kuwa mama kwa malaika wawili – Asia Brown
na Ice Brown.