
MCHUNGAJI mmoja ameibua wasiwasi kwa wanandoa katika mitandao ya kijamii baada ya kufichua kile alichokiita kama utabiri wake kuhusu kitakachotokea katika ndoa nyingi mwezi Aprili.
Katika video hiyo ambayo imezua gumzo
zikiwa zimesalia siku chache kukamilisha mwezi Machin a kukaribisha rasmi mwezi
Aprili, mchungaji huyo alionekana akitoa utabiri bila kutetereka kwamba ndoa
nyingi zitasambaratika sana mwezi huo wa 4.
Kwa mujibu wake, ndoa nyingi
zitavunjika kwa sababu wanaume wengi watapoteza nguvu za kiume ghafla, huku
wanawake wakilazimika kutafuta huduma kwa wanaume wengine wenye nguvu.
“Kuanzia mwezi wan ne 2025, wanaume
nguvu za kiume zitapotea ghafla. Asilimia kubwa ya wanaume, nguvu za kiume
zitakuwa zikipotea ghafla. Na ndoa nyingi sana zitaingia kwenye shida,” alihubiri huku waumini
wakimtumbulia macho wasijue cha kufanya.
Kando na wanaume kupoteza nguvu za
kiume ghafla, mchungaji huyo pia alisema hilo litawaweka wanawake walioko
kwenye ndoa katika hatari ya kulazimika kuchepuka ili kutafuta kukidhi haja za
miili yao.
“Wanawake wengi watatoka kwenye ndoa
zao kwenda kutafuta wanaume wengine. Lakini yule mwanaume mpya atakayempata,
baada ya kuwa naye kwa muda mfupi naye nguvu za kiume zitakuwa zimekata,” aliendeleza kupakua
injili.
Alisema kwamba wanawake wengi kutokana
na kutompata mwanaume mwenye nguvu za kiume kikidhi mahitaji yao ya tendo la
ndoa, watakuwa wanazunguka kutoka kwa mwanamume mmoja kwenda kwa mwingine –
yote hayo kuanzia Aprili mosi!
Kama ni kweli, basi ni mwaka ambao
wanawake watakuwa wanawayawaya kama kuku aliyekatwa kichwa wakitafuta kukidhi
mahitaji ya miili yao.
“Mwanamke huyo ataenda tena kwa
mwanamume mwingine na kumkuta huyo pia nguvu za kiume hana. Ni mwaka ambao
wanawake watakuwa wanawayawaya.”
Hata hivyo, mahubiri yake
hayakukamilika bila kutoa suluhisho kwa utabiri huo, haswa akiwalenga wanawake.
“Aprili 2025 ukimuona mumeo hana nguvu
za kiume, tulia hapo hapo. Hapo utakapotaka kukimbilia penyewe pia
hazitakuwepo. Muombee mumeo!” pasta alishauri.
Alisema kwamba mwaka 2025 ni wa
mwanamke kuchukua usukani wa kufanya toba ya maombi kwa ajili ya ustawi wa
familia zao.
“Mwaka 2025 ni mwaka wa mwanamke
kusugua goti, kwenda kwenye nyumba za ibada kwa ajili ya kuombea afya ya mume
wako,” alimaliza waumini wakimpigia makofi.
Tazama video hiyo hapa;