
RAIS William Ruto ametumua mfano wa mama kutembea katika safari ya ujauzito mpaka kutotoa mwana katika kuelezea safari ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo humu nchini.
Akizungumza na wanahabari wa vituo
mbalimbali kutoka eneo pana la Mlima Kenya kuelekea ziara yake ya kimaendeleo
katika eneo hilo, Ruto alisema kwamba baadhi ya Wakenya wanadhani hakuna
maendeoe katika miradi aliyoianzisha miezi ya nyuma lakini ukweli ni kwamba
miradi hiyo inaendelea.
Kiongozi wa nchi alisema kwamba haiwezekani
mradi uanzishwe leo na kukamilika le oleo kwani ni safari ndefu kama ya kubeba
mimba hadi kujifungua.
“Ukioa bibi akuambie nitakuzalia mtoto,
pengine hawezi kukuzalia wiki ya kwanza kwa sababu hilo haliwezekani. Lazima yale
mambo yafanyike halafu ndio tungoje ndio mtoto apatikane,” rais alisema huku
akicheka.
Pia alitumia mantiki ya mfano wa mtoto
kuenda shuleni, akisema kuwa hawezi fika shuleni siku ya kwanza na kufunzwa
kila kitu, akirejelea dhana kwamba kila kitu kinahitaji muda ili kukamilika au
kudhihirisha maana halisi.
“Unajua hata ukienda shuleni unapatiwa
somo, unafanya mwigo hapo katikati halafu kuna siku ya mtihani mkuu, kama ni
shule za sekondari mtihani mkuu ni baada ya miaka 4, si ndio?”
Mkuu wa nchi alisema kwamba iko haja
watu kumpa muda kufanya kazi kulingana na manifesto yake na kwamba muda wa
kumhukumu haujafika kwani amesalia na miaka 2 kuelekea kukamilika kwa muhula
wake wa kwanza.
“Sasa nataka kuwauliza, si mtihani huu
wa barabara za Mau Mau nilisema nitamaliza? Si mtihani uko 2027? Hizi barabara
za Mau Mau uniulize siku hiyo kama hazitakuwa zimekamilika ujenzi. Na kama
nitakuwa sijafanya si wananchi watajua jinsi ya kufanya?” aliongeza.
Ruto ameanza rasmi ziara yake ya siku 5
katika eneo pana la Mlima Kenya akitarajiwa kuzuru kaunti 9 za eneo hilo.
Hii ni mara ya kwanza kwa rais
kutembelea eneo hilo tangu kutimuliwa ofisini kwa aliyekuwa naibu wake, Rigathi
Gachagua.