MWANAMKE mwenye umri wa miaka 28 katika mkoa wa Kusini nchini Zambia ameripotiwa kufa baada ya kile kilichosemekana kama ni kutumia mafuta ya upako kutoka kwa mtu mmoja anayejiita nabii wa Mungu.
Kifo cha mwanamke huyo ambacho kilijiri
wikendi iliyopita kimezua tafrani katika taifa hilo lenye asilimia kubwa ya
madhehebu ya Kikristo yanayoendeshwa na watu binafsi wanaojitambulisha kama
watumishi wa Mungu.
Kesi hiyo iliripotiwa katika Kituo cha
Polisi na babake mwanamke huyo, chanzo kiliripoti.
Baba huyo aliripoti kuwa siku ya Ijumaa,
bintiye alianza kujisafisha na kutapika muda mfupi baada ya kuchukua maji na
mafuta hayo kutoka kwa mchungaji wa kanisa moja la kiroho mwenye umri wa miaka
37 hadi saa 04:00 asubuhi ya leo ambapo hatimaye alifariki.
Afisa wa polisi aliyejua kisa hicho
amethibitisha kuwa nabii huyo anayedaiwa alikwenda na kutembelea eneo hilo kwa
lengo la kuwaponya wagonjwa wa kila aina ya maradhi.
Pasta huyo anasema mtu ambaye sasa ni
marehemu alimwendea Ijumaa Aprili 4, 2025 kutafuta matibabu ya utasa.
Anasema siku hiyohiyo ya saa 13:00
alipewa "maji matakatifu na mafuta ya kupaka" kunywa kama matibabu ya
hali yake lakini baadaye alianza kutapika na kujisafisha hadi leo asubuhi saa
02:00 usiku alipokimbizwa katika Zahanati ya Makuyu ambako baadaye alifariki
majira ya saa 04:00.
Maafisa walizuru eneo la tukio, na
kuchukua maiti kwa uchunguzi na kumkamata mshukiwa kwa uchunguzi kuhusu kisa
hicho.