
ALIKIBA ametangaza tarehe rasmi ya tamasha lake la kuadhimisha miaka 20 ya safari yake kwenye mawimbi ya muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram,
Alikiba Alifichua kwamba tamasha hilo la kipekee litafanyika Aprili 19 visiwani
Zanzibar ambapo makumi ya wasanii watakuwepo kutumbuizia mashabiki.
Akionyesha maandalizi ya tamasha hilo,
Alikiba alichapisha moja ya video akifanya mazoezi na Live band, akisema kwamba
mashabiki wataburudishwa moja kwa moja na wasanii usiku wote.
“Ninajiandaa kwa miaka 20 ya ALIKIBA. Je,
uko tayari?” Alikiba aliuliza kupitia Instagram.
Baadhi ya wasanii ambao amethibitisha
kuwaalika katika mkesha huo wa kusherehekea miaka 20 kwenye muziki ni pamoja na
Darassa, Whozu, Chege Chigunda, Dulla Makabila miongoni mwa wengine.
Kuelekea siku yake kuu, msanii huyo
amekuwa akizindua miradi mbalimbali ambayo amenukuliwa akisema kuwa ni katika
mkondo huo wa kuadhimisha miaka 20.
Mwezi Machi mwaka jana, Alikiba
alizindua kituo chake cha runinga, Crown Media kuadhimisha miaka 20.
Katika hafla iliyosheheni nyota wengi,
Kiba alisema analenga kuwafikia watu wengi iwezekanavyo kupitia chombo chake
kipya cha Crowns Media kitakachojumuisha kituo cha televisheni, redio, vyombo
vya habari vya digitali na matukio mbalimbali.
Ali Kiba sasa anaungana na mwimbaji
mwingine wa Tanzania Diamond, ambaye anamiliki jumba la habari kamili la Wasafi
Media.
Diamond ni miongoni mwa waimbaji
waliotamba sana nchini Tanzania na kwa hakika Afrika Mashariki, lakini kwa
hakika ugomvi wake na Ali Kiba umewafanya wasambaratike zaidi.
Bila kujali, wote wawili wanafurahia
mafanikio makubwa ndani na nje ya muziki.