logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Yesu akiwa duniani hakuwahi ingia katika nyumba ya maskini hata siku moja – pasta

Alidai kwamba Yesu wakati wa huduma yake ya miaka 33 duniani, hakuna hata siku moja alimtembelea mtu maskini na kuingia katika nyumba yake.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani14 April 2025 - 16:26

Muhtasari


  • Kasisi huyo alitoa marejeo ya kibiblia ili kuendeleza hoja yake juu ya hili, kwani alitoa mifano ambapo Yesu aliwatembelea matajiri pekee.
  • Mchungaji David Ibiyeomie alishikilia kwamba Mkristo hapaswi kuwa na mawazo duni, kama Kristo tayari alikufa ili kuhakikisha kwamba wao si maskini.

Mchungaji David Ibiyeomie

MHUBIRI mashuhuri, kutoka Nigeria Mchungaji David Ibiyeomie anaamini kwamba Yesu hakuwahi kuwapenda maskini hata kidogo wakati wa enzi zake duniani.

Haya ni kulingana na klipu moja ya mahubiri yake tata ambayo imekuwa ikikosolewa kwenye mitandao ya kijamii.

Mchungaji huyu katika klipu hiyo, alidai kwamba Yesu wakati wa huduma yake ya miaka 33 duniani, hakuna hata siku moja alimtembelea mtu maskini na kuingia katika nyumba yake.

Kasisi huyo alitoa marejeo ya kibiblia ili kuendeleza hoja yake juu ya hili, kwani alitoa mifano ambapo Yesu aliwatembelea matajiri pekee.

Mchungaji David Ibiyeomie alishikilia kwamba Mkristo hapaswi kuwa na mawazo duni, kama Kristo tayari alikufa ili kuhakikisha kwamba wao si maskini.

Aliwacha wakiristo changamoto ya kutoa kifungu chochote kwenye Biblia kinachoesimulia au kumuonyesha Yesu akitembea na kuingia katika nyumba ya maskini.

Alisema kwa sehemu…

"Yesu hakuwahi kumtembelea maskini yeyote nyumbani, soma biblia yako. Maana yake anachukia umaskini.”

Mchungaji huyo alizama zaidi kutolea mifano ya baadhi ya wahusika kwenye Biblia ambao Yesu aliwatembelea na kutoa sababu zake kwa nini anaamini wahusika hao hawakuwa maskini.

“Cheki, alimtembelea Lazaro, hawakuwa masikini, walikuwa wakimpa chakula. Alimtembelea mwenye dhambi aitwaye Zakayo ambaye alikuwa tajiri; niambie yule maskini Yesu aliingia nyumbani kwake; anachukia umaskini maana yake, anachukia watu ambao ni maskini. Alikufa kwa ajili yako usiwe maskini wa akili ili uje kanisani. lakini huruhusiwi kubaki maskini…”

Mahubiri yake yalizua mchanganyiko miongoni mwa waumini wa mitandaoni, baadhi wakimtaka kuelezea kifungu kinachosema kwamba itawawia vigumu matajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni kama ngamia kuingia kwenye tundu la sindano.

Wengine walimpinga kwa Kauli yake kwamba Lazaro alikuwa tajiri wakisema kwamba alikuwa maskini wa kutupiwa makombo ya chakula sakafuni.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

@Bobbydbobo aliandika: "Hawa wachuuzi sha. Yesu sawa na kusema "Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu." Watataka kuendeleza mazungumzo ya nyumbani juu ya ufanisi kwa faida yao wenyewe na kisha kupotosha Biblia.”

@AtarodoScotch alisema: "Ikiwa hii ni kweli. Kwa heshima zote 'Wewe ni Wazimu Bwana' kwa sababu Watin iwe hivi 😤🙄"

@VivienVivico aliandika: “Je, Lazaro rafiki yake alikuwa tajiri? Je, mama-mkwe wa Petro alikuwa mwanamke tajiri?”

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved