
BOSI wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide, Harmonize ameonyesha maendeoe ya jinsi anavyozidi kujiweka mbali na maisha ya nje, akisema kwamba lengo lake ni kuwa na kila huduma nyumbani kwake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alichapisha
video akionyesha kukamilika kwa chumba chake cha mazoezi ya kunyanyua vyuma
ambacho kimeshehedi vifaa vyote vya gym.
Harmonize alisema kwamba katika orofa ya juu, ana studio kwa
ajili ya kufanya kazi zake za muziki na chini ana gym hivyo itakuwa vigumu sana
kwa watu kukutana naye nje.
Msanii huyo Alifichua kwamba itakuwa nadra sana kutangamana
na watu nje ya jumba lake la Konde Village, akisema kwamba kitu pekee ambacho
kitamfanya kutoka na anapoenda kutafuta matibabu kwani hospitali tu ndiyo
hajaweka katika moja ya vyumba vyake.
Kwa mashabiki wake ambao wangependa kuchukua fursa muhali
watakapomkuta, Harmonize aliwataka kufanya kumbukumbu njema naye ikitokea
wamekutana nao nje, kwani kuonekana kwake kutakuwa kwa uchache wa ajabu.
“Itakuwa ghali sana
kuniona pale nje, hebu tutengeneze kumbukumbu nzuri ikitokea tumekutana kwa
maana sasa nina karibia kila kitu ndani. Kitu pekee ambacho pengine sina kwa
sasa ni hospitali,” Harmonize aliandika.
Msanii huyo alitoa angalizo zaidi kwa yeyote ambaye angependa
kujiunga naye kwenye mazoezi katika gym yake ya nyumbani, akisisitiza kwamba
watoto wa kike tu ndio watakaokubaliwa.
“Nimerahisisha kila kitu,
Konde Fitness iko tayari nyumbani kwangu, na ningependa kuwa na waalikwa lakini
wawe warembo pekee. Mnaona gym iko chini na studio iko juu, juu ya dunia. Tag warembo
wale ambao wanapenda kushiriki mazoezi ya gym waambie gym ya baba iko tayari,” Harmonize aliongeza.