
SAA chache baada ya YouTuber Oga Obinna kudai kwamba alipatwa na mshangao kugundua mchekeshaji Mulamwah amemblock katika mitandao wa Instagram, Mulamwah ameibuka na kukiri kufanya hivyo, huku akitoa sababu.
Obinna Alifichua kulishwa block na Mulamwah wakati alipokuwa
akijibu sababu ya kutotokea kusimama naye katika shoo yake binafsi ya kwanza
iliyofanyika wikendi iliyopita.
Obinna alidai kwamba hakuwa na taarifa kuhusu kufanyika kwa
shoo ya vichekesho ya Mulamwah na alipodokezewa, ndipo aliamua kumtafuta
Instagram kuona lakini akapatwa na butwaa kugundua hawezi mfikia.
“Binafsi mimi sina bifu
lolote na Mulamwah. Japo niligundua ile siku ya shoo yake kwamba ameniblock. Tulikuwa
mjini nikaambiwa Mulamwah ako na shoo nikashtuka kuenda kuangalia nikapata niko
blocked,” Obinna alieleza.
“Pia sikuwa najua kama
shoo yake ilikuwa inafanyika ile siku kwa sababu ningeenda. Sababu kama
nilikuwa sina shughuli mbona nisiende. Kwa wengine [ambao hawakuenda] siwezi
jua. Lakini pengine walikuwa wameshikika, unaona siku kama za Jumamosi huwa na
shughuli nyingi, angeweka kama Jumapili au Jumatatu labda wangetokea,” Obinna aliongeza.
Hata hivyo, Mulamwah alijitokeza na klipu ya Obinna akicheka
wakati Dem wa FB alipokuwa anamueleza jinsi watu walikuwa wanamdhihaki mwanawe,
Oyando Jr mitandaoni.
Katika klipu hiyo iliyochapishwa na Mulamwah kutoka kwa
Weekly Show ya Obinna na Dem wa FB – kipindi ambacho kilifikia mwisho mwaka
jana, alimkumbusha kwamba chanzo cha yeye kulishwa block kilitokana na hapo.
“Mwenye alienda haja
kubwa njiani husahau lakini mwenye alikanyaga katu hawezi kusahau. Hapa ndipo
ulikulia tofali,’ Mulamwah aliandika.
Kwenye klipu hiyo, Dem wa FB alikuwa anajaribu kumueleza
Obinna jinsi watu walimkejeli mtoto wa Mulamwah mitandaoni, baadhi
wakimfananisha na muigizaji marehemu Papa Shirandula.
Obinna alionekana kujaribu kuzuia kicheko chake kwa dhihaka
hiyo, lakini inaonekana kujibeba kwake kwenye muktadha mzima kulimkera Mulamwah
kufikia hatua ya kumblock.