"Ananiweza sana!" Zuchu aeleza sababu ya kurudiana na Diamond baada ya kum'cheat na Fantana

"Yeye kama kaamua kuwa hivyo, wacha awe hivyo. Afanye kwa uwezo wake, siku nitajiona nimechoka nitamuacha,” Zuchu alisema.

Muhtasari

•Zuchu alikiri kuwa alivunja vitu ndani ya nyumba ya Diamond baada ya kuona sehemu ambapo bosi huyo wa WCB alimbusu mshirika huyo wake kwenye YFA2.

•“Naweza kuwa nimefungwa macho na mapenzi lakini sidhani niko chini sana kuwa kipofu. Nahisi kama maelezo aliyonipa ilinipa muda kuifuta lakini ilifika hatua nikaamua kumsamehe," Zuchu alisema.

Zuchu asema hawezi kumwacha Diamond
Zuchu asema hawezi kumwacha Diamond
Image: Screengrab//Zuchu

Malkia wa Bongofleva, Zuhura Othman almaarufu Zuchu amekiri kuwa alijawa na ghadhabu na kusababisha fujo baada ya kumuona bosi yake Diamond Platnumz akimbusu Fantana kwenye filamu ya Young, Famous na African .

Katika mahojiano na Wasafi Media, Zuchu alikiri kuwa ni kweli alivunja vitu ndani ya nyumba ya Diamond baada ya kuona sehemu ambapo bosi huyo wa WCB alimbusu mshirika huyo wake kwenye YFA2.

Alifichua kuwa wakati huo alikuwa akifanya usafi ndani ya nyumba ya Diamond alipoona video hiyo kwenye Snapchat.

“Kweli nilivunja vitu. Ilitokea. Nilikuwa nimekasirikasana. Niliona rafiki yangu amevuka mipaka. Hayo sio mambo unafanya kwenye runinga rafiki,” Zuchu alisimulia.

Aliendelea, “Kwa kweli nilikuwa nyumbani kwake. Nilikuwa bize nikiosha nyumba na nilikuwa napanga glasi nikawa nimeshika simu nikaingia snapchat. Niliona ile scene, nikawa najiuliza kama ni video ya kweli nikasema hapana nimekataa.”

Mwimbaji huyo wa kibao ‘Sukari’ alifichua kuwa aliwahi kukutana na Fantana hapo awali wakati wa kurekodi kwa filamu hiyo nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo alisema kuwa tukio la Diamond kumbusu mwimbaji huyo wa Ghana lilimpata kwa mshtuko na kumfanya akasirike.

"Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona scene hiyo kama kila mtu mwingine. Moyo wangu ulivunjika. Sikujua la kufanya na nilikuwa nikimpigia simu, nadhani alikuwa ikulu siku hiyo ikawa hapokei simu, nadhani kwa sababu alikuwa bize,” alisema.

Zuchu alieleza kuwa ni baada ya bosi wake kukosa kuchukua simu yake ndipo alifanya fujo kutokana na hasira kwani hakuweza kuzungumza na mtu yeyote.

Alikiri kwamba alipiga kelele tu huku akivunja vitu ndani ya nyumba ya bosi huyo wake  kabla ya kuondoka na vitu vyake.

“Baadaye alikuwa akinipigia simu na sikuwa nikipokea simu zake. Sikutaka tu kuzungumza naye. nilikuwa nimemalizana naye,” alisema..

Malkia huyo wa bongofleva alisema kuwa Diamond aliendelea kujaribu kumpigia simu hadi akapokea mida ya saa tisa usiku na bosi huyo wa WCB akamweleza kwanini hakuwa akipokea simu yake.

“Kuna changamoto nyingine, nadhani sijui ananiweza sana. Nimekuwa mrahisi sana kwake. Sikuwa hivi, niamini, huwa sipatiani nafasi za pili. Sijui kwa nini na yeye,” alisema.

Alifichua kuwa alimtumia Diamond ,ambaye anasisistiza ni rafiki wake tu, video hiyo ya busu ambaye na kumfahamisha kuwa hiyo ndiyo sababu ya hasira yake.

“Naweza kuwa nimefungwa macho na mapenzi lakini sidhani niko chini sana kuwa kipofu. Nahisi kama maelezo aliyonipa ilinipa muda kuifuta lakini ilifika hatua nikaamua kumsamehe… Nadhani ni vizuri kwenye mapenzi mtu akawa huru kufanya chochote anachotaka.Kwa hivyo yeye kama kaamua kuwa hivyo, wacha awe hivyo. Afanye kwa uwezo wake, siku nitajiona nimechoka nitamuacha,” Zuchu alisema.