Mpenzi wa Brian Ogana azungumzia madai ya ujauzito

Muhtasari

• Kumekuwa na minong’ono mitandaoni kuhusiana na mpenzi wa muigizaji Brian Ogana kuwa mjamzito.

• Madai haya ya wajasusi wa mitandaoni yanakuja mwezi mmoja tu baada ya muigizaji huyo wa kipindi maarufu cha Maria kumtambulisha mpenzi wake mitandaoni kwa jina la Dyder Abdalla

Brian Ogana na mpenziwe
Image: HISANI

Kumekuwa na minong’ono mitandaoni kuhusiana na mpenzi wa muigizaji Brian Ogana kuwa mjamzito.

Madai haya ya wajasusi wa mitandaoni yanakuja mwezi mmoja tu baada ya muigizaji huyo wa kipindi maarufu cha Maria kumtambulisha mpenzi wake mitandaoni kwa jina la Dyder Abdalla na tangu hapo wamekuwa wakionesha mapenzi yao mubashara kwenye mitaa ya mitandao.

Katika video moja iliyosambazwa mitandaoni na paparazi, mkanda huo wa video unaonesha kabisa mpenzi wa Ogana akiwa na ujauzito mkubwa.

Saa chache baada ya kufuja kwa video hiyo, Dyder amejitoa wazi na kukana madai hayo huku akisema kwamba yeye pia madai hayo ya ujauzito anayasikia kama ambavyo watu wengine wanayasikia.

"Mimi mwenyewe naskia kama nyinyi, nipeni miezi tisa tutajua," aliandika Dyder

Watu walimjia juu na ikabidi ameweka wazi Zaidi kwa ufafanuzi. 

"Naona kila mtu anasema kuhusu hii ishu ya ujauzito na mimi mwenyewe sijui, hebu tafuteni ufafanuzi Zaidi na mnipe taarifa Zaidi, sijui, huenda ikawa kweli" 

Siku za hivi karibuni mpenzi wa Dyder, Brian Ogana alionekana na kitambaa cha Arafat, maarufu sana kwa waislamu, jambo ambalo lilizua madai kuwa amebadilisha dini na kujiunga dini ya kiislam. Dyder aliweka bayana kwamba Ogana hajabadilisha dini ili kufanikisha njama yake kumuoa.