Hatimaye Tunda na Whozu wameanza upya mapenzi yao

Muhtasari

• Uvumi wa kurudiana ulianza wikendi iliyopita ambapo mwanadada Tunda alipakia picha ya pamoja akimtakia kheri njema ya siku ya kuzaliwa Whozu na pia maisha marefu.

Whozu, Tunda na mwanawe
Whozu, Tunda na mwanawe
Image: Tunda Cappuccino (Instagram)

Fununu mitandaoni ni kwamba msanii mchekeshaji Whozu na mpenziwe Tunda hatimaye wameruadina baada ya mahusiano yao kusemekana yalisambaratika miezi michache iliyopita.

Wapenzi hao wawili wanadhaniwa kurudiana baada ya siku za hivi karibuni majasusi wa mitandaoni na mapaparazi kuwafuatilia kwa ukaribu na kubaini kwamba wamekuwa na maongezi yenye tija, si tu kwa kukutana bali hata kwenye mitandao ya kijamii.

Hili hata lilibainika kabisa baada ya Tunda kumtakia maisha marefu msanii Whozu.

Ikumbukwe wawili hao wamejaaliwa na mtoto mmoja ambaye wamempa jina Lolla. Uvumi wa kurudiana ulianza wikendi iliyopita ambapo mwanadada Tunda alipakia picha ya pamoja akimtakia kheri njema ya siku ya kuzaliwa Whozu na pia maisha marefu.

Hivi Mjuzi, Whozu alitoa tamko la kutaka kina mama wapewe heshima iliyotukuka kwani bila wao hakuna mwendelezo wa kizazi kingine.

Tamko hilo lake kutaka heshima kwa kina mama idumu lilishabikiwa kwa wingi na wanadada wanaofanya vizuri maishani ambapo wengi waliitaja kauli hiyo kuwa ishara mojawapo ya kukomaa kiakili.