Harmonize ampa Diamond tuzo baada ya kushinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume 2021

Muhtasari
  • Harmonize ampa Diamond tuzo baada ya kushinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kiume 2021
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Harmonize

Harmonize ni msanii maarufu wa Kitanzania wa Bongo anayejulikana kwa nyimbo zake zinazovuma na video zake bora.

Ni baba wa msichana mmoja mrembo aitwaye Zuu Konde. Harmonize ni miongoni mwa msanii nchini Tanzania anayeishi maisha ya kifahari kwani kutokana na wadhifa wake inaonekana .

Yeye ni mshawishi wa chapa, balozi wa chapa, mwanamitindo, Mkurugenzi Mtendaji, mfanyabiashara, mwandishi wa nyimbo, mwimbaji wa nyimbo.

Harmonize kwa muda wa miaka mitatu iliyopita hajakuwa akishirikiana na bosi wake wa zamani ambaye aliunga mkono muziki wake alipoanza Diamond Platnumz .

Hii ni baada yakutoka kwenye lebo ya Wasafi na kuanzisha label yake ya Konde Music.

Hata hivyo jana Harmonize alionyesha kuwa na maelewano mazuri naye alipokuwa akifanya shoo. Alisimama na kumwita diamond kuwa msanii bora zaidi Tanzania.

Alisema kuwa anajua kuwa hana maelewano naye lakini jembe linapaswa kuitwa jembe.

Huku akituzwa tuzo ya kuwa mwanamuziki bora wa kiume mwaka wa 2021, alikabidhi tuzo hilo kwa msanii Diamond huku akisema sio vyema kubeba tuzo tatu ilhali Diamond hajapata tuzo yeyote.