'Yuko 'broke' hana pesa,'Ringtone asema huku akisisitiza anayajua mengi kuhuru Eric Omondi

Muhtasari
  • Ringtone hatimaye amekiri kwamba Eric Omondi anaishi maisha duni na kwamba hana pesa
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE, ERIC OMONDI

Mcheshi Eric Omondi alivuma sana wikendi iliyopita baada ya kuwa kwenye drama isioeleweka na staa wa bongo wa Tanzania Harmonize.

Wawili hao walikejeliwa sana mitandaoni na wanamitandao,uku drama hiyo ikimsababishia Harmonize kukamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kileleshwa.

Ringtone hatimaye amekiri kwamba Eric Omondi anaishi maisha duni na kwamba hana pesa.

Ringtone kwenye mahojiano alisema kuwa Erick ana deni na pia aliongeza kuwa ametuma maombi yote ya mkopo kutoka kwa programu mbalimbali za maombi ya mkopo ikiwa ni pamoja na Tala.

Eric Omondi bado hajajibu video yake inayosambaa mtandaoni lakini ni dhahiri kwamba atafanya hivyo bila muda.

Ringtone Apoko pia badala yake anamfahamu Eric Omondi zaidi na hata marafiki zake.

Eric Omondi amekuwa akitoa wito kwa vyombo vya habari kucheza muziki wa Kenya, huku akifanya kazi nyuma ya pazia na Harmonize ili kukuza muziki wa Tanzania.

Siku ya JUmapili Eric alidai kwamba baada ya kuenda kumtembelea Harmonize polisi alimchapa ngumi.

Pia aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko alisema kwamba hakumshtaki staa huyo.