'Angalieni hawa wajinga,'Kate Actress amkemea mwandishi aliyesema amesafiri ng'ambo kufanyiwa upasuaji

Muhtasari
  • Anajulikana kwa ustadi wake wa ajabu wa kuigiza hasa kwa tabia yake ya hasira na ujasiri
Catherine Kamau
Catherine Kamau
Image: INSTAGRAM

Catherine kamau anayejulikana kwa jina la kisanii kama Kate Actresssi mwigizaji wa Kenya tu bali pia mwanamitindo, mtu mashuhuri,  mtayarishaji wa maudhui kwa youtube na tiktok.

Alipata umaarufu baada ya kushiriki katika kipindi cha 'mother-in-lwa kwenye runinga ya Citizen.

Anajulikana kwa ustadi wake wa ajabu wa kuigiza hasa kwa tabia yake ya hasira na ujasiri.

Kazi yake imekuwa ikiimarika haswa baada ya kupewa kandarasi na netflix.

Ameshiriki katika filamu ya 'Disconnect' ambayo ni ya kenya ya Netflix kama vile mastaa wengine kama vile Brenda wairimu na Nick Mutuma wameshiriki pia.

Licha ya kuwa mtu wa umma, yeye ni mama na vile vile ni mama wa kujivunia kutokana na picha mbalimbali anazopakia mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii.

Hapo awali, alipeleka huzuni yake kwenye mitandao ya kijamii baada ya gazeti moja kuandika habari zake. kusafiri nje ya nchi kufanya upasuaji kwa sababu ya unene.

Alikanusha madai hayo huku akiendelea kulitusi gazeti na waandishi kwa kutoa habari za kupotosha kwa mashabiki wake.