'Tuko pamoja,'Frankie afichua hawajaachana na Corazon Kwamboka

Muhtasari
  • Frankie alisema kuwa bado anamchumbiana na  Corazon Kwamboka
Frankie na Corazon Kwamboka
Image: INSTAGRAM

Frankie amezua tafrani tena mtandaoni hii ni baada ya kuamua kuweka wazi uhusiano wake na baby mama wake Corazon Kwamboka.

Akizungumza katika mahojiano  Frankie alisema kuwa mambo yote ambayo watu walikuwa wakiyaona mtandaoni yalikuwa kiki tu hajawahi kuwa na maelewano mabaya na Corazon Kwamboka, na wamekuwa pamoja.

Frankie alisema kuwa bado anamchumbiana na  Corazon Kwamboka, na hawakuwahi kuachana, uhusiano wao bado upo na wanajipanga kwenda kisiwani hivi karibuni.

Frankie alisema kuwa wakati mwingine ni vizuri sana Kuwachanganya adui zako kwa sababu watu walikuwa wanajali sana biashara zao, na hivyo wakaamua kudanganya kwamba wameachana.

Frankie alisema kuwa anawashukuru mashabiki wake kwa kumpa  na kumtia moyo na sasa amewatambua marafiki zake wa kweli, na marafiki feki na Imekuwa uzoefu mzuri.