Sitawahi msahau ex wangu Wolper-Juma Jux akiri

Muhtasari
  • Huku akiwa kwenye mahojiano na Wasafi, akijibu swali ni ex yupi bora zaidi maishani mwake kati ya Jackline Wolper na Jackie Cliffe alisma kwamba hatawahi msahau Wolper
Juma Jux
Juma Jux

Hata baada ya kuvuma sana mitandaoni wiki chache zilizopita baada ya madai ana uhusiano na mwanasosholaiti Huddah Monroe Juma Jux amekiri hatawahi msahau mmoja wa ex wake.

Huku akiwa kwenye mahojiano na Wasafi, akijibu swali ni ex yupi bora zaidi maishani mwake kati ya Jackline Wolper na Jackie Cliffe alisma kwamba hatawahi msahau Wolper.

"Eh, nani alikuwa bora zaidi wa zamani? Unataka nifanye wapi hii? Ni lazima nichague? Dah! Hii ni ngumu wanaume, Hii ​​ni hivyo. ngumu kwa sababu kila hatua ninapitia kwenye maisha yangu kila moja ni muhimu, Ila kama ningechagua ningesema ni Wolper. I will never forget my ex-Wolper."

Akijibu picha ya Huddah Monroe na aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee, almaarufu Vee Money kwenye skrini, Jux aliulizwa aeleze anapendelea nani.

"Kusema kweli wote ni warembo na wa ajabu kwa namna yao. Wasichana wote ni pisi ni wazuri hapa. Vanessa ni mrembo, Huddah, ni mrembo pia. Unataka nichague nani mzuri zaidi?"

Jux alisema, "Wote wawili ni warembo, kila mmoja ana plus/faida zake kwa njia tofauti."

Lil Ommy hakushawishika na kumtaka Jux azikadirie kwa asilimia.

Jux alisema, "Waah, wote wana plus yao, kuna vitu wamezidiana. Kuna vitu navipenda kila mmoja wao kivyake, kitu ninavyo penda kwa Huddah, kuna vitu ninavyopenda kwa Vee."