Nilitoka kwenye uhusiano wangu na Nelly Oaks Desemba-Akothee afichua

Muhtasari
  • Hatimaye Esther Akothee amejitokeza kuzungumzia uhusiano wake na Nelly Oaks na kufichua siku aliyoachana naye
Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: Instagram///AKOTHEE

Hatimaye Esther Akothee amejitokeza kuzungumzia uhusiano wake na Nelly Oaks na kufichua siku aliyoachana naye.

Akizungumza katika mahojiano na Presenter Ali, Akothee alisema kuwa huwa hatangazi kutengana bila kupona kutoka kwake kwanza.

Akothee alisema kuwa aliweka hadharani talaka hiyo kwa sababu tayari alikuwa amepona kutokana nayo na alihisi ulikuwa wakati mwafaka wa kuweka mambo hadharani.

Akothee alisema ukweli ni kwamba alimtupa Nelly Oaks mnamo Desemba 2021 na sababu iliyomfanya aamue kufanya hivyo ni kwa sababu hakuwa na furaha na nguvu zao hazikuwa zikilingana hivyo akajikuta akijituma sana.

Akothee alisema kuwa ana uhusiano kadhaa na anachothamini zaidi ni utulivu wake wa akili na pia nguvu ambazo wote huleta katika uhusiano huo.

Akothee alisema yuko single na anafurahia maisha yake.

"Mapenzi ni matamu, na ni matamu unapopatana na mtu anayefaa, mapenzi yatakupata kwa njia moja au nyingine,lakini cha muhimu ni nguvu ambayo mnaleeta wenye uhusiano wenu wa mapenzi

Mnapoachana kila mtu huwa ameumia kutoka kwenye uhusiano huo, naweza kusema nilitoka kwenye uhusiano wangu na Nelly Oaks Desemba," Akothe alifichua.

HUku akizungumzia tasnia ya burudani nchini, ambayo inaonekana kudhoofika kila kuchao alisema kuwa;

"Nchini kenya tuna talanta nyingi sana, lakini jinsi ya kukuza hizo talanta ndio changamoto, kila msanii anapitia changamoto zake na za muziki

Shida na mashabiki wa humu nchini wanashabikia wasanii ktoka nchi za nje kwani wasanii wa humu nchini wanakabaliana na changamoto cngu nzima, ndio maana nilikuwa nimekuja kukutana na Ezekiel Mtua."