Wachana na watoto wangu nilikuachia Jimal-Amira amshambulia Amber Ray

Muhtasari
  • Haya basi tunapofikiria kwamba vita vyao vimefika kikomo,au vimekwisha mambo yanabadilika na wawili hao kuanzisha vita tena
Amira
Image: Hisani

Sio siri wala habari za kushangaza kwamba mwanasosholaiti ndiye sababu ya mwanabiashara Jimal na mkewe Amira kuachana.

Haya basi tunapofikiria kwamba vita vyao vimefika kikomo,au vimekwisha mambo yanabadilika na wawili hao kuanzisha vita tena.

Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa Amira amemuonya Amber Ray dhidi ya kuingilia katika maisha ya watoto wwake.

Kulingana na Amira wikendi iliyopita hakuwa nyumbani, na aliporejea mwanawe alimwambia kwamba Amber Ray alikuwa anamuita wapige picha pamoja, alipotembelea makazi ambayo Amira anaishi.

Zaidi ya yote Amira alimuonya Amber dhidi ya kuwa na uhusiano wa na wanawe, na kumwambia kwamba alimuachia Jimal.

"Mtu amwambie Amber Ray wakati mwingine akija Yamin asivuke mipaka, nilipokuwa siyuko wikendi iliyopita alishinda kumuita mwanangu Shamir, ambaye alikuwa anacheza aende wapige picha pamoja

Aliniambia haya niliporudi nyumbani, sikiza kaa mbali na watoto wangu, nilikuachia Jamal inapokuja kwa watoto wangu tutakosana na tutaona damu," Aliandiika Amira.

Amber Ray hajajitokeza kukana au kukubali madai ya Amira.