'Nitakufanya uwe mwanamke mwenye furaha,'Willy Paul ammezea msanii Jovial mate

Aiidha amesema kwamba mtu hapaswi kuhukumiwa kutokana na maisha yake ya awali

Muhtasari
  • Msanii huyo kupitia ujumbe wake alimwambia Jovial kuwa akipata nafasi ya kuwa mpenzi wake atampa raha
Willy paul
Willy paul
Image: hisani

Msanii maarufu nchini Willy Paul kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, amekuwa akimtumia jumbe msanii Jovial.

Siku ya Alhamisi msaniii huyo alimwanndikia Jovial ujumbe ili akubali awe mpenzi wake.

Msanii huyo kupitia ujumbe wake alimwambia Jovial kuwa akipata nafasi ya kuwa mpenzi wake atampa raha.

Aiidha amesema kwamba mtu hapaswi kuhukumiwa kutokana na maisha yake ya awali,kwani hamna mtu ambaye ni mkamilifu maishani.

"@jovial_ke atleast kuwa na utu. Sikatai watu wanasema mimi ni bwana mkunaji, I don't know why.. in life lazima kila mtu anachoka na anaamua kutulia mimi hapa naomba nitulie na wewe. Nobody is perfect so we shouldn't judge someone based on his or her past.. Man is to error, but If you give me this chance then for sure I'll make you the happiest woman on the planet earth,'Willy Paul Aliandika.