(+video) Mwanaume afungwa jela miaka 5 kwa kumroga mtoto wa ndugu yake

Mwanaume huyo alisemekana kufuga nyoka ndani mwake ambayo kwa macho ya kawaida ilikuwa inaonekana kama jiwe.

Muhtasari

• Baada ya mtoto kupata ukichaa, familia ilienda kwa mganga kupigiwa ramli iliyoonesha amefanyiwa ushirikina.

• Baadaye walielekea kanisani ambapo pia maombi yalitoa matokeo hayo na kuamua kumuuliza mtuhumiwa ambaye alikiri na hivyo wakampeleka mahakamani.

Mahakama
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Kwa muda mrefu kumekuwa na msemo kwamba dola haitambui kesi zinazohusiana na ushirikina au ulozi.

Lakini hali ni tofauti katika nchi Jirani Tanzania baada ya mahakama moja kufanay kufuru ya kusikiliza kesi ya aina hiyo na hakika kumpata mtuhumiwa na makosa ya kumfanyia vitendo vya ushirikina mtoto wa nduguye.

Habari hiyo imezungumziwa sana katika ukanda wa Afrika mashariki kwani mara nyingi ilikuwa inadahamika kwamba kesi za ushirikina mara nyingi hazina Ushahidi na hivyo ni vigumu kusikilizwa achia mbali hata kutiliwa maanani na taasisi za kisheria.

Mahakama hiyo iliyopo Wilaya ya Ludewa ilimhukumu kifungo cha miaka 5 jela jamaa mmoja kwa jina John Chale mwenye umri wa miaka 60 kwa kosa la kumfanyia vitendo vya kishirikina mtoto wa mdogo wake Videana Chale mwney umri mbichi wa miaka 18 tu na kupelekea kupata ukichaa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo ya wilaya alisema kwamba mahakama ilielezwa binti huyo alipatwa na ukichaa ambapo wazazi walifanya juhudi za kumpeleka kwenye mtibabu wa asili ambaye alitambika na kupiga ramli iliyotoa majibu kwamba binti alitiwa ulozi na jamaa huyo.

Familia hiyo kwa kutoamini ramli ya mganga, walimpeleka tena kanisani ambako ilisemekana kwamab huko nako majibu hayakutofautiana na ya mganga, jambo lililowashrutisha kumuuliza mshatakiwa kwa kile walisema kwamba amekuwa akikumbwa na kesi za aina hiyo mara si moja na ilisemekana alikuwa anamiliki nyoka ndani ya nyumba yake anayeonekana kama jiwe na watu.

Aidha mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa hilo ndipo baba mzazi wa mtoto huyo Hekima Chale akaamua kupeleka jambo hilo katika vyombo vya sheria ambako mtuhumiwa huyo alikana lakini baada ya kufanyika upelelezi na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili mahakama ilijilidhisha kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo pasipo shaka yoyote ikiwa ni kinyume cha sheria ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

 

Baada ya kupatikana na hatia, Mwendesha mashtaka wa serikali aliiomba mahakama kumpatia mshtakiwa huyo adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa jamii kwani vitendo vya kishirikina vimekuwa vikisababisha migogoro katika familia na jamii kwa ujumla ndipo mahakama hiyo ikatoa hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela.

 

Kwa upande wa utetezi wake mtuhumiwa huyo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu hiyo kwakuwa ni kosa lake la kwanza, anategemewa na familia na pia ni mgojwa wa kisukari lakini mahakama ilimtaka kutumikia kifungo hicho.