Jamal Roho Safi ajipata pabaya baada ya kumrushia vijembe aliyekuwa mkewe

Kulingana na ujumbe wake Jamal alikuwa akiwashauri mashabiki wake kuwachumbia wenzi ambao wanajua kusamehe mkikosana.

Muhtasari
  • KUlingana na baadhi ya mashabiki wake ni kuwa ujumbe huo ulikuwa unamwelekea aliyekuwa mke wake Amira
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Image: Instagram//JimalRohosafi

Mwanabiashara Jamal Roho Safi, kwa mara nyingine amejipata upande mbaya na mashabiki wake baada ya kupakia ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram.

KUlingana na baadhi ya mashabiki wake ni kuwa ujumbe huo ulikuwa unamwelekea aliyekuwa mke wake Amira.

Jamal alivuma sana mitandaoni baada ya kumuoa mwanasosholaiti Amber Ray.

Kulingana na ujumbe wake Jamal alikuwa akiwashauri mashabiki wake kuwachumbia wenzi ambao wanajua kusamehe mkikosana.

"Unapochumbia ili kuoa chumbia mwenzi ambaye anajua kusamehe na wala sio mtu ambaye anavuta mambo kutoka Nazareth mpaka Galilee," Aliandika Jamal.

Baada ya ujumbe wake mashabiki walitoa hisia tofauti na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

leila.hassaan: The question is if she did exactly what you did showing some PDA. Will you forgive her easily or drag it as well? Start with being a good carin friend first everything will fall into places accordingly InshaAllah.

njuguna_caro: Talk to her direct, nyumba kubwa😂😂😂

muthoni12346: Ni musimu wa nyanya ?maembe iliisha

vickywambui98: And when you're marrying marry a faithful partner 😂

elenalynes: You should forgive 70×77 times ....ni kama wewe ulisamehewa hadi zikaisha 😂😂why do you need extra forgiveness

missgachugi: Sio by force akuforgive. Ulichoma tuu sana. Kwanza ile video ya Kempinski 🥺. Mwiba wa kujichoma…