Fahamu sifa ambazo mbunge Peter Salasya anazingatia kwa mwanamke

Juu kwenye orodha yake ya sifa za anazozingati ni mwanamke awe mcha Mungu.

Muhtasari

•Salasya aliweka wazi kuwa mwanamke anayetafuta lazima pia awe tayari kumuunga mkono katika taaluma yake ya kisiasa na kijana pia.

•Pia aliongeza kuwa anataka kuwa na watoto 10.

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya Salasya afichua sifa za mwanamke ambaye anamtafuta
Peter Salasya Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya Salasya afichua sifa za mwanamke ambaye anamtafuta
Image: Facebook

Takriban miezi miwili baada ya kukitwaa kiti cha Ubunge cha Mumias Mashariki kilichomezewa mate na wengi, Peter Salasya amefahamisha ulimwengu kuwa sasa anatafuta mwanamke wa kutulia naye.

Mbunge huyo mwenye umri wa ujana ambaye alivunjwa moyo mwaka wa 2017 alipopoteza azma yake ya ubunge anaonekana kupona na sasa anaendelea na msako wa kumtafuta msichana mzuri wa kufunga naye ndoa.

Hata hivyo, yeye hafanyi iwe rahisi kwa wasichana.

Salasya (ambaye alipata umaarufu kutokana na mwanzo wake duni na ukweli kwamba alikuwa na Ksh 500 tu mfukoni wakati wa kuapishwa kwake) wakati wa mahojiano ya hivi majuzi aliangazia sifa chache ambazo anatafuta kwa mke.

Juu kwenye orodha yake ya sifa za anazozingati ni mwanamke awe mcha Mungu.

Kisha akaenda kuelezea sifa zingine chache ambazo zingemgusa mwanamke.

Kwanza, mbunge huyo mwenye umri wa ujana aliweka wazi kuwa mwanamke anayetafuta kujaza nafasi ya mkewe lazima pia awe tayari kumuunga mkono katika taaluma yake ya kisiasa na kijana pia.

Kisha akaendelea kusisitiza kwamba mwanamke anayefaa kujaza nafasi hiyo lazima awe na uwezo wa kuwasiliana vizuri na watu wa vijijini, kupunguza msako wake kwa wale ambao wanaweza kustawi vijijini.

"Natafuta tu mwanamke anayeomba sana, msichana mdogo sana, msichana makini, msichana msaidizi, anayeonekana na lazima awe na uwezo wa kuzungumza na watu wa mashambani.

"Mwanamke msomi kati ya miaka 23-26. Hakuna hata mmoja ambaye ataendelea kuchungulia kwenye simu yangu kwa sababu simu za baba ziko na scandals mob (simu za wanaume zimejaa kashfa).

"Pia awe tayari kukaa kijijini, akichunga (kuchunga) jimbo, kama uko tayari kuungana nami twende kutafuta kura?" Salasya alisema.

Pia alisema kuwa yeye ni mtu mwenye maarifa.

"Mimi ni mtu mwenye maarifa... Kwani naeza pelekwa pelekwa hivi. Mimi ni mbunge na unajua nimewaaminisha watu kuwa mimi ni mtu mwenye akili sana. Nina nguvu," aliongeza.

Salasya alifichua kuwa tangu achaguliwe kuwa mbunge, wanawake wamekuwa wakimtumia jumbe na picha kwenye simu yake.

Pia aliongeza kuwa anataka kuwa na watoto 10, akifichua kuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake wa zamani katika muda wa wiki moja.