Betty Kyallo azama tena kwenye dimbwi la mahaba

"Mapenzi ni kitu kizuri," alisema.

Muhtasari

•Betty alichapisha picha yake akiwa ameshikilia shada la maua, na kusema hilo ndilo tukio maalum la wiki yake.

•Hivi majuzi Nick alisema anampeza mpenzi wake wa zamani, akimtaja kama mtu mzuri.

Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Mtangazaji na mjasiriamali maarufu Betty Kyallo amedokeza kuhusu kuwa mahusiano mapya.

Hivi majuzi, mama huyo wa mtoto mmoja alichapisha picha yake akiwa ameshikilia shada la maua, na kusema hilo ndilo tukio maalum la wiki yake.

"Mapenzi ni kitu kizuri," aliandika.

Mahusiano ya mwisho ya hadharani ya Betty Kyallo yalikuwa na wakili Nick Ndeda.

Wawili hao walipoachana, Betty alisema walikuwa na mitazamo tofauti ya masuala fulani ya kimaisha.

"Katika mahusiano, ni kuhusu kufahamiana. Ilifika mahali ambapo tulikuwa hatuna mwelekeo sawa upande na uhusiano."

Hivi majuzi Nick alisema anampeza mpenzi wake wa zamani, akimtaja kama mtu mzuri.

"Ninakosa mambo fulani fulani, sitasema uwongo. Nishati nzuri na yote," Nick alisema.