'Sitaolewa,'Nasra asema huku akifichua kitu anachopeza sana kutoka kwa Rashid

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, katika kipindi cha Q&A alifichua kwamba hataolewa hivi karibuni.

Muhtasari
  • Huku akitangaza kuachana kwa kwa mashabiki,Nasra alisema kwamba alipigania uhusiano wao,na kumtakia kila la kheri Rashid katika maisha yake

Mchekshaji Nasra Yusuf siku ya Jumapili alifichua kwamba hawayuko pamoja na mume wake mchekeshaji mwenzake Rashid.

Huku akitangaza kuachana kwa kwa mashabiki,Nasra alisema kwamba alipigania uhusiano wao,na kumtakia kila la kheri Rashid katika maisha yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, katika kipindi cha Q&A alifichua kwamba hataolewa hivi karibuni.

Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza iwao ataolewa tena.

"Apana sitaolewa tena, nimemaliza, itagharimu pesa nyingi ili kubadili akili yangu,"Nasra alijibu.

Pia alisema kwamba huwa hawazungumzi na mumewe, licha yake kuwa na picha zake kwenye mitandao ya kijamii.

Mchekeshaji huyo alisema picha hizo ni sehemu ya maisha yake, kwa hivo hawezi kuzifuta kutoka kwenye mitandao.

Shabiki mwingine alimuuliza nini haswa anapeza kwenye ndoa yake, na majibu yake yalikuwa kama yafuatavyo;

"Tulikuwa marafiki sana, nitapeza jokes na tabasamu yake, kwa kweli ni mwanamume mzuri tayari kusaidia mtu yeyote, mimi na yeye hatukuelewana lakini ni mzuri,"Alisema Nasra.