Daddy Owen azungumzia madai ya kutoka kimapenzi na 'shabiki' wake

Akizungumza na Word Is, Owen alisema Eve ni rafiki tu.

Muhtasari

•Madai kwamba wawili hao wako kwenye mahusiano yaliibuka baada ya mashabiki kugundua kuwa walikuwa wamechapisha picha iliyopigwa katika eneo moja.

•"Katika picha hiyo, tulikuwa tu tukibarizi pamoja na watu wengine," Owen alisema.

Daddy Owen na Eve Maina
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen amekanusha madai kwamba anachumbiana na rafiki yake wa karibu Eve Maina.

Madai kwamba wawili hao wako kwenye mahusiano yaliibuka baada ya mashabiki kugundua kuwa walikuwa wamechapisha picha iliyopigwa katika eneo moja.

Katika picha yake, Eve alisema yuko tayari kuachilia mwaka wa 2023.

"Sipunguzi kasi kwa mtu yeyote." alisema.

Owen alisema Mungu huwapata watu hata katikati ya matatizo yoyote. Akizungumza na Word Is, Owen alisema Eve ni rafiki tu.

"Anachumbiana na sina nia ya kuchumbiana naye. Tumekuwa marafiki kwa muda mrefu," alisema.

"Katika picha hiyo, tulikuwa tu tukibarizi pamoja na watu wengine."

Mwezi Oktoba 2022, Owen alichapisha picha iliyoonyesha akiwa na Eve, huku wakiwa wamevalia mavazi yanayolingana na akimrejelea kama shabiki.

Alifanya utani kuhusu picha hiyo na kusemaEve aliweka uso wa ukali.