"Nimetosheka sana" Mpenziwe Wema Sepetu afichua sababu za kumpenda kupitiliza

Wema aliweka wazi kwamba mpenzi huyo wake ndiye sababu ya furaha kubwa aliyo nayo.

Muhtasari

•Wasanii hao wawili walitumia siku hiyo kusherehekeana na kuhakikishiana kuhusu upendo wao kwa kila mmoja.

•Whozu alitumia siku ya Wapendanao kueleza baadhi ya sababu za kumpenda Miss Tanzania huyo wa zamani.

Wema Sepetu na Mpenzi wake Whozu
Image: INSTAGRAM// WHOZU

Wapenzi maarufu wa Bongo, muigizaji Wema Sepetu na mwimbaji Whozu waliadhimisha siku ya Wapendanao kwa njia maalum.

Wasanii hao wawili walitumia siku hiyo kusherehekeana na kuhakikishiana kuhusu upendo wao kwa kila mmoja.

Wema aliweka wazi kwamba mpenzi huyo wake ndiye sababu ya furaha kubwa aliyo nayo siku za hivi majuzi.

"Mkumbato wangu shweet, mpenzi wangu wa kukumbatia, sababu ya tabasamu langu lisiloisha❤❤❤,"  muigizaji huyo alimwandikia Whozu kwenye mtandao wa Instagram na kuambatanisha na picha yake.

Mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Diamond Platnumz aliendelea kumuita mpenziwe maneno matamu ya mahaba kama vile; Valentine's wangu, Furaha yangu ya kweli, Wangu wa pekee, Faraja yangu, Chaguo langu, Msiri wangu, Mshunu Wangu, miongoni mwa majina mengine mengi.

"Naapa mbele ya Mungu nakupenda sana Chibaba wangu Wallahy," alisema.

Whozu kwa upande wake alitumia siku ya Wapendanao kueleza baadhi ya sababu za kumpenda Miss Tanzania huyo wa zamani.

Mwimbaji huyo alidokeza kuwa mahusiano yake na Wema Sepetu yanahusisha upendo, heshima, amani na kujaliana.

"Mapenzi yanaweza kuwa mazuri sana kama utampata anaekupenda, kukuheshimu na kukujali. Asante mungu kwa kuniweka sehemu tulivu, Nisiwe Muongo Napata Amani ya moyo napata Furaha, Natabasamu naenjoy mapenzi yangu..😊🙏🏽

Nimetosheka sana na Chimama Wangu. Acha tu nikupende siku zote nibaki na wewe milele My Valentine❤️," alisema.

Whozu alichapisha video nzuri yake na mpenziwe wakishiriki wakati mzuri na kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa mapenzi ya kweli.

Huku akijibu ujumbe wa mpenziwe, Wema alimhakikishia kuwa yeye ndiye mshindi wa moyo wake na kutabiri mapenzi yao ni ya milele.

"Ila Amore unapenda ligi mpenzi wangu...😍😍😍 Itakuaje sasa😂😂😂 Haiya basi ushachukua ushindi. Naskia raha kuwa wako mshindi wangu. Wangu hadi milele," Wema alimwambia mpenziwe.

Wema na Whozu waliweka mahusiano yao wazi mwaka jana baada ya kuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu.